Kisinda aanza Kariakoo Dabi

KOCHA Nasreddine Nabi amemuanzisha Tuisila Kisinda kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi dhidi ya watani zao Simba.
Tuisila anacheza mechi yake ya kwanza ya dabi tangu alipoondoka nchini akicheza sambamba na Jesus Moloko wakicheza winga.
Wakati eneo la ulinzi kaanza na kipa Dijgui Diarra, Djuma Shabani, Kibwana Shomari na walinzi wa kati ni Yanick Bangala na Dickson Job.
Katikati ameanza na Khalid Aucho akicheza sambamba na Feisal Salum ‘Fei Toto’ huku eneo la ushambuliaji akianza na Fiston Mayele alisaidiana na Stephan Aziz Ki.
Benchi kuna Abutwalib Mshery, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Gael Bigirimana, Zawadi Mauya, Farid Mussa, Dickson Ambundo, Denis Nkane na Herietie Makambo.