Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa skendo za ngono, talaka zawatesa mastaa kinoma

Giggs na Stacey, skendo ya kutoka na shemeji yake ndio ilivunja ndoa ya staa huyu wa Man United na mkewe.

LONDON, ENGLAND. MAPENZI magumu. Mastaa wa soka usiowane wanatesa sana uwanjani lakini wakati mwingine mambo nyumbani yanakuwa magumu.

Ndoa zinakuwa ngumu na mwishowe huishia katika talaka. Wafuatao ni mastaa ambao walitembeza talaka kwa wapenzi wao. Wengi wao ni kwa makosa yao wenyewe.

Dani Alves and Dinora Santana (2008-11)

Hii hapa ni talaka ya ajabu sana. Licha ya staa huyu wa kimataifa wa Brazil alimtembezea mkewe talaka lakini mpaka leo mkewe ni wakala wake. Miaka saba baada ya talaka yao, Dinora Santa amebakia kuwa mtu muhimu katika maisha ya kazi ya staa huyu wa PSG.

Julai 12, 2017 siku ambayo Alves alitambulishwa kwa mashabiki wa PSG Uwanja wa Parc des Princes, Alves alifuatana na watoto wake wawili na mkewe Mhispaniola Manna Joana Sanz. Hata hivyo, mtu ambaye alikuwa amefanya mazungumzo yote ya kufikia mkataba na PSG alikuwa mtalaka wake Dinora. Mama huyu aliamua kutojitokeza siku hiyo.

James Rodriguez na Daniela Ospina (2010-17)

Staa wa kimataifa wa Colombia ambaye anakipiga kwa mkopo wa miaka miwili Bayern Munich akitokea Real Madrid. Talaka yake ilikuja karibuni. Alifunga ndoa na Daniela Ospina ambaye ni dada wa kipa wa Arsenal, David Ospina Desemba 24, 2010. Waliona katika Mji wa Mdellin Colombia huku Daniela akiwa na umri wa miaka 18 tu.

Baada ya hapo walikwenda kuishi Ureno ambako James alikuwa akikipiga katika Klabu ya Porto. Mtoto wao wa kwanza alizaliwa Machi 29, 2013 wakamuita jina la Salome.

Hata hivyo, wakati James akielekea kukipiga Bayern Munich walitangaza kuachana kwa kile kilichodaiwa Daniela hakutaka kwenda naye Ujerumani. Juu ya hilo ilizuka habari James alikuwa na uhusiano wa pembeni na mwanamitindo maarufu Ulaya, Helga Lovekaty.

Ryan Giggs na

Stacey (2007-17)

Staa wa zamani wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Wales, Ryan Giggs ambaye kwa sasa ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Wales kuna wakati jina lake halikubanduka katika kurasa za mbele za magazeti ya Uingereza kwa sababu ambazo hazikuwa za kisoka.

Giggs alikuwa na mkewe, Stacey, 40 na watoto wawili ilipobainika kuwa kumbe kwa miaka minane alikuwa na uhusiano na mke wa mdogo wake, Rhodri Giggs. Baadaye mwanamama huyo aliamua kubwaga manyanga ambapo Giggs alilazimika kumpa kiasi cha Pauni 40 milioni katika utajiri wake kama fidia ya kuvunjika kwa talaka hiyo.

Wakati alipoteuliwa kuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Wales, baba yake, Danny alisikika akilishutumu vikali Shirikisho la Soka la Wales kwa kumteua mtu asiye mwaminifu katika kazi hiyo. Danny alidai familia isingeweza kumsamehe Giggs kwa kitendo alichokifanya.

Djibril Cisse na

Jude Cisse (2005-12)

Staa wa zamani wa Liverpool na Timu ya Taifa ya Ufaransa. Ndoa yake na mwanamke wa Wales, Jude ilivunjika mwaka 2012 baada ya miaka minane ya ndoa hiyo.

Wawili hao walikuwa na watoto watatu pamoja, na kabla ya hapo kila mmoja alikuwa na mtoto mmoja katika uhusiano wake wa awali. Kuna ripoti ziliibuka baadaye Jude alikuwa anatoka kimapenzi na staa wa Arsenal, Henrikh Mkhitaryan.

Ashley Cole na Cheryl Cole

(2004-10)

Ilikuwa ndoa maarufu Uingereza. Mmoja alikuwa staa wa soka akitamba na Arsenal, Chelsea na Timu ya Taifa ya England wakati mwingine alikuwa staa wa muziki. Walioana mwaka 2004 lakini wakajikuta wakitengana miaka sita baadaye Februari 23, 2010 kwa kile kilichodaiwa Ashley Cole alikuwa akijirusha na wanawake wengine. Waliachana rasmi Septemba 3, 2010. Kwa sasa Cole ana watoto wawili ambao amezaa na mwanamitindo wa Kiitaliano Sharon Canu.

Ahmed Mussa na Jamila (2017)

Staa wa kimataifa wa Nigeria ambaye ni nahodha wa timu hiyo. Akiwa na Leicester City, Aprili 2017 polisi waliitwa katika nyumba ya Musa kuamua ugomvi kati yake na mkewe Jamila.

Baada ya siku chache walikubaliana kuachana huku wakiwa na watoto wawili. Mwezi mmoja baadaye Musa alirudi kwao Nigeria kwenda kumuoa mwanamke aliyeitwa Juliet Ejue Mei 23, 2017. Inadaiwa ugomvi wa Musa na Jamila ulitokana na staa huyo kuposti katika mtandao wa Instagram picha ya Juliet huku akiandika ‘Malkia wangu’.

Ray Parlour na Karen (1998-2001

Parlour alimuoa mke wake, Karen mwaka 1998. Waliachana mwaka 21 wakiwa na watoto watatu. Julai 2004 walikubaliana kumaliza mzozo wa masuala ya pesa ambapo ilikubalika Karen apewe nyumba mbili na kiasi cha Pauni 250,000 lakini hawakukubaliana katika suala la pesa ya malezi. Parlour aliahidi kutoa kiasi cha Pauni 120,000 kwa mwaka kwa madai ingetosha kwa mahitaji ya watoto na mwanamke lakini hata hivyo Karen alitaka zaidi. Mahakama ilitaka Parlour atoe kiasi cha Pauni 212,000 kwa mwaka lakini pande zote hazikukubali. Karen aliona ndogo wakati Parlour aliona kubwa. Mahakama ilimuongezea Karen mpaka kiasi cha Pauni 440,000 achilia mbali kiasi cha Pauni 250,000 ambacho kingelipwa kila mwaka. Walikubaliana. Kwa sasa Parlour yupo katika uhusiano na mpenzi wake, Joanne Jones, tangu mwaka 2001 huku wakiwa na watoto wawili pamoja.

Thierry Henry

Staa mwingine wa zamani wa Arsenal ambaye naye ndoa yake iliingia katika majnga. Septemba 2007, Mahakama iliamuru mke wa Henry, Claire Merry, 27 wakati huo apewe talaka ya haraka kutokana na tabia mbovu za mumewe aliyekuwa na uhusiano na wanawake wengine.

Inadaiwa baada ya miaka minne ya ndoa, Claire alifumania meseji za mapenzi za staa huyo katika simu yake. wawili hao walikubaliana kulimaza tatizo hilo kupitia kwa wanasheria wao ambao Claire inasemekama alilipwa kiasi cha Pauni 10 milioni na staa huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa. Inadaiwa Claire aliweka wazi alikuwa anafanya kazi nzuri kabla ya kukutana na staa huyo aliyeng’ara zaidi akiwa na Arsenal. Wakati wanaachana Henry alikuwa anachezea Barcelona huku akilipwa kiasi cha Pauni 130,000 kwa wiki na utajiri wake ulikuwa unakadiriwa kufikia Pauni 25 milioni.