Kisa Simba, Dieng, Tau wapigwa 'stop' Ahly

Zikiwa zimebaki siku 10 kwa Simba kuwavaa mabingwa wa Afrika Al Ahly ya Misri kwenye Africa Super League Oktoba 20, timu hiyo imewazuia wachezaji wake wawili Percy Tau wa Afrika Kusini na Aliou Dieng wa Mali kujiunga na timu zao za Taifa kwa ajili ya mashindano hayo.
Nyota Percy Tau aliitwa kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi Eswatin Oktoba 13 na 17 dhidi ya Ivory Coast huku Dieng angeivaa Uganda na Saudi Arabia.
Mabingwa hao mara 10 wa Ligi ya Mabingwa Afrika watatua nchini Oktoba 17 mwaka huu kuivaa Simba kwenye mechi ya ufunguzi Uwanja wa Mkapa.