Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa matokeo mabovu Namungo, Kaze ajiuzulu

Baada ya kupoteza pointi tatu jana dhidi ya Singida Big Stars  kwa kichapo cha mbao 3-2, Kocha Mkuu wa Namungo, Cedrick Kaze  amejiuzulu kupitia taarifa aliyoindika kwenye akaunti yake ya Instagram 

“Nimeamua kuanzia leo kujiuzulu kama Kocha Mkuu wa Namungo; napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana Uongozi, wafanyakazi wenzangu wa benchi la ufundi na wachezaji kwa ushirikiano wao na kujitolea.

“Nimalizie kwa kuwashukuru mashabiki ambao wamekuwa wakiniunga mkono kila wakati.

Naitakia timu kila la heri kwa siku zijazo.”


Kaze aliliambia Gazeti la Mwanaspoti kabla ya mechi dhidi ya Singida mchezo huo ndiyo umeshikilia kibarua chake Namungo;  "Haitakuwa rahisi lakini maandalizi niliyoyafanya na wachezaji wangu ni kuhakikisa tunakuwa bora na kutumia vizuri uwanja wa nyumbani ili kujihakikishia pointi tatu muhimu ambazo zimeshika kibarua change.”

Namungo kwenye mechi sita ilizocheza imepoteza tatu na kutoka sare tatu ikianza na Kagera Sugar (1-1), Mashujaa (0-0), Yanga (1-0), KMC (1-1) na walikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania na Singida.