Kipa Tausi FC aanika mikakati yake

Muktasari:
- Uganda ilikuwa kati ya timu zilizocheza mechi za kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake ikiiondosha Ethiopia kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare ya 2-2.
BAADA ya kuitumikia timu ya taifa ya Uganda kwenye michezo miwili ya kufuzu WAFCON mwakani, golikipa wa Tausi FC, Ruth Aturo amesema anatamani kuisaidia timu hiyo kupanda daraja msimu ujao.
Uganda ilikuwa kati ya timu zilizocheza mechi za kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake ikiiondosha Ethiopia kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare ya 2-2.
Katika mechi hizo golikipa huyo alicheza zote mbili na kuonyesha umahiri wa kudaka penalti moja kati ya tano zilizopigwa kwenye lango lake.
Aturo ambaye anaichezea Tausi iliyopo Ligi Daraja la Kwanza alisema kama mchezaji anatamani kuandika historia nzuri ya kuipandisha timu hiyo Ligi Kuu.
Aliongeza kuwa kutokana na usajili mkubwa uliofanywa na timu hiyo ikiwamo kuleta kocha wa kigeni ni wazi wakipambana wanaiona nafasi hiyo.
“Ligi ya Tanzania nzuri ina ushindani mkubwa watu wa hapa wanapenda michezo, timu yetu iko vizuri na tunaendelea kukomaa.”