Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Mtibwa ageuka lulu

Muktasari:

  • Kipa huyo aliyemaliza na clean sheets nne za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, inadaiwa ameanza mazungumzo na baadhi ya klabu za Namungo, Kagera Sugar, JKT Tanzania na Dodoma Jiji, kwani malengo yake kwa sasa ni kupata changamoto mpya.

KLABU za Namungo FC, JKT Tanzania, Kagera Sugar na Dodoma Jiji zimeanza kumfuatilia kipa wa Mtibwa Sugar, Toba Kutisha kwa ajili ya kupata saini yake, baada ya nyota huyo kudaiwa kwa sasa anaangalia pia mazingira mapya msimu wa 2026-2027.

Kipa huyo aliyemaliza na clean sheets nne za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, inadaiwa ameanza mazungumzo na baadhi ya klabu za Namungo, Kagera Sugar, JKT Tanzania na Dodoma Jiji, kwani malengo yake kwa sasa ni kupata changamoto mpya.

Hatua ya nyota huyo kutafuta changamoto mpya inatokana na Mtibwa Sugar kushuka daraja kutoka Ligi Kuu hadi Championship msimu wa 2025-2026, baada ya kumaliza nafasi ya 15 na pointi 27, ikiungana na KMC FC iliyomaliza mkiani na pointi tisa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mratibu wa Namungo, Ally Suleiman alisema baada ya msimu kumalizika watapokea ripoti nzima ya benchi la ufundi kwa ajili ya kuangalia maeneo ya kuboresha, ingawa malengo makubwa ni kusajili wachezaji wenye ubora.

“Msimu wa 2025-2026, ulikuwa ni mgumu sana kwetu kwa sababu tulikwepa nafasi ya kushuka daraja na hata kucheza mechi pia za Play-Off ya kubakia, tutafanya tathimini vizuri kwa kuangalia maeneo muhimu ya kuyaboresha zaidi,” alisema Suleiman.

Hata hivyo, Mwanaspoti linatambua Mtibwa Sugar inafanya mazungumzo ya kumuongezea mkataba kipa huyo, ingawa mojawapo ya changamoto kubwa inayoweza kumshawishi kuondoka ni kutokana na kikosi hicho kushuka daraja na kushiriki Championship.

Licha ya Mtibwa Sugar kushuka daraja, ila Toba ni miongoni mwa makipa bora wa kikosi hicho akishindania nafasi na nyota mwenzake, Constantine Malimi ambaye msimu wa 2025-2026, katika Ligi Kuu Bara alimaliza pia akiwa na clean sheets nne.