Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kings yatwaa ubingwa BBall Kitaa Arusha

Muktasari:

  • Kocha Mkuu wa timu ya Kings, Raymond Yusuph alisema ni furaha kubwa kutwaa ubingwa huo ni ishara wamerudi katika kiwango kinachotakiwa na ushindani.

Arusha: Kings imetwaa ubingwa wa mashindano ya kikapu ya B’Ball Kitaa kwa kuifunga Scorpion kwa pointi 70 kwa 60 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, Arusha.

Kocha Mkuu wa timu ya Kings, Raymond Yusuph alisema ni furaha kubwa kutwaa ubingwa huo ni ishara wamerudi katika kiwango kinachotakiwa na ushindani.

Kwa ushindi huo timu ya Kings licha ya kuzawadiwa Kombe, pia itaghalamiwa safari ya kuelekea Jijini Dar es Salaam kwenye michuano ya B’Ball Kitaa ya kitaifa itakayofanyika hapo badaaye mwaka huu.

 Kings iliingia katika hatua hiyo baada ya kuilaza Hooperz katika mchezo wa nusu fainali kwa vikapu 58 kwa 42, huku timu ya Scorpion ikiilaza Palllot kwa vikapu 66 kwa 47.

Ofisa michezo wa jiji la Arusha, Benson Maneno alisema  ni vyema vijana kuendela kujikita kwenye michezo kama sehemu ya ajira.

Kwa sasa mkoa wa Arusha unajiandaa na mashindano ya Kanda yatakayofanyika kwa siku nne Mkoani Tanga kuanzia Novemba Mosi mwaka huu, na timu mbili za juu zitakwenda kuwakilisha mashindano ya Mabingwa ya kanda Jijini Dar es salaam.