Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kina Kikoti freshi, ishu usafiri

Muktasari:

  • Takribani wiki mbili sasa wachezaji wa Namungo watatu na kiongozi mmoja wa timu hiyo wamesota nchini Angola baada ya kupimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona, hatimaye jana wamepimwa tena na kukutwa wamepona.

HATIMAYE WACHEZAJI watatu wa klabu ya Namungo waliosalia nchini Angola kutokana na kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona, wanatarajia kurejea nchini Jumamosi Februari 27 au Jumatatu Machi Mosi baada ya kupimwa na kukutwa wamepona jana.
Februari 13 msafara wa Namungo wakiwa Uwanja wa ndege, Angola wakiwafuata wapinzani wao De Agosto katika mchezo wa kombe la Shirikisho walikumbana na sintofahamu baada ya wachezaji wao watatu na kiongozi mmoja kupimwa na majibu yakaonyesha wana corona na kuwekwa karantini.
Iliwaradhimu Namungo kurejea Tanzania na kuwaacha wachezaji hao Khamis Faki, Fredy Tangalu, Lucas Kikoto pamoja na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Omary Kaaya.
Hassan Zidadu ambaye ni Mwenyekiti wa timu hiyo yenye maskani yake Ruangwa mkoani Lindi amesema wanamshukuru Mungu jana walipewa taarifa kutoka Angola kuwa watu wao wako salama kwa sasa hivyo wamewaachia waweze kurejea Tanzania.
"Serikali ya Angola ilisema itaweza kuwaachia wakionekana hawana corona, ila jana mchana walipimwa walionekana wako poa, lakini passport zao ziko uhamiaji," amesema.
Amesema Serikali ya Angola hapo awali ilihaidi kuwa gharama za kuwasafirisha watu hao wanne zitakuwa juu yao lakini cha kushangaza wamebadilisha tena maamuzi hayo.
"Wametuambia kuwa hawatawalipia tena, na kama unavyojua huko Angola kuna ndege mbili tu Jumamosi na Jumatatu hivyo kama uongozi tunahakikisha tunapambana tunafanya taratibu za kuwarejesha hapa nchini, iwe Jumamosi au Jumatatu," amesisitiza.


MCHEZO WA LEO
Leo saa 10:00 jioni Namungo atakuwa mwenyeji katika Uwanja wa Chamazi kukabiliana na Agosto Zidadu amesema, mpaka sasa wameiva na kila kitu kipo sawa asilimia 95.
"Wachezaji wako vizuri hata benchi la ufundi kilichosalia kwa sasa ni hizo tano tu, ila tuko vizuri sana kwa mchezo huo,"
Namungo mchezo uliopita alishinda mabao 6-0, mchezo uliopigwa uwanja huo huo baada ya CAF kutaka mechi zote mbili kupigwa Tanzania kutokana na changamoto iliyojitokeza Angola.