Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichobaki Bara ni vita ya nafasi na noti

Muktasari:

  • Yanga ndio inayoongoza msimamo ikiwa na pointi 73, ikifuatiwa na Simba yenye alama 72, kila moja ikisaliwa na mechi tatu tofauti na klabu nyingine 14 zilizosalia za ligi hiyo zenye michezo miwili kila moja, huku Azam na Singida Black Stars zikifuata nyuma yao zikichuana katika nafasi ya tatu na nne.

LIGI Kuu Bara imesaliwa na mechi 19 ikiwamo Dabi ya Kariakoo kabla ya kufungwa kwa msimu huu, huku vita ya ubingwa ikisalia kwa vigogo Simba na Yanga, ilihali nafasi nyingine imebaki kuwa ni vita ya nafasi ya pesa za wadhamini wa ligi hiyo iliyoasisiwa mwaka 1965.

Yanga ndio inayoongoza msimamo ikiwa na pointi 73, ikifuatiwa na Simba yenye alama 72, kila moja ikisaliwa na mechi tatu tofauti na klabu nyingine 14 zilizosalia za ligi hiyo zenye michezo miwili kila moja, huku Azam na Singida Black Stars zikifuata nyuma yao zikichuana katika nafasi ya tatu na nne.

Azam ina pointi 57 baada ya mechi 28, tatu zaidi ya ilizonazo Singida yenye 53 ikiwa pia na idadi ya mechi kama hizo ambapo zinaviziana kuhakikisha nani anayemaliza katika nafasi ya tatu kwa lengo la kuvuna mamilioni ya fedha kutoka kwa wadhamini.

Vita ya nafasi ya tatu kati ya Azam na Singida BS inaendelea kutokana na namna timu hizo zinavyofukuzana kwenye ukusanyaji wa pointi katika mechi mbili zilizobaki achana na hilo kuna hili la mgao wa fedha kwenye nafasi hiyo.

Wakati bingwa wa Ligi Kuu atapata Sh500 milioni kutoka Azam Media, mbali na zile za mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Benki ya NBC, timu itakayoshika nafasi ya pili itavuna Sh250 milioni, ya tatu Sh225 milioni na ya nne Sh200 milioni. Hapo ndipo vita ya Azam na Singida ilipo kwani kila moja inaipigia nafasi ya tatu kwa lengo la kuvuta mkwanja wa maana.

Azam ipo nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 57 ikiwa imecheza mechi 28 na mechi mbili mkononi ili kukamilisha msimu ikiwa na mchezo dhidi ya Tabora United nyumbani na Fountain Gate ugenini, wakati SBS pia imecheza mechi 28 na kukusanya pointi 53 ina mechi dhidi ya Dodoma Jiji ugenini na nyumbani dhidi ya Prisons.

Hata katika nafasi kuanzia ile ya tano hadi ya 14 zote zina fedha kutoka kwa wadhamini wa maudhui ya matangazo Azam Media na hapo ndipo klabu zinazotoleana macho kwa vile tayari KenGold na Kagera Sugar zimeshaaga rasmi ligi kwa kushika nafasi mbili za mwishoni.

Kwa mujibu wa mkataba wa Azam Media mgao wa nafasi kuanzia msimu wa 2021-2024, ukiacha nafasi nne za juu, timu inayomaliza ya tano inavuna Sh65 milioni, ilihali anayeshika nafasi ya sita atapata Sh60 milioni, huku zinazocheza play-offs nazo hazitoki patupu, kwani kuna Sh20 milioni inayozisubiri.


WASIKIE MAKOCHA

Kocha wa Azam, Rachid Taoussi alisema;  “Sio rahisi kushinda mechi zote, tuna uwezo wa kumfunga kila mpinzani anayekuja mbele yetu, lakini kuna wakati tukubali hatuwezi kushinda kwa kila mechi. Tunahitaji umakini zaidi katika mechi zijazo kwa sababu hakuna mchezo utakaouwa rahisi.”

“Hatma ya nafasi yetu ipo mikononi mwa Singida katika mchezo wetu unaofuata na tunahitaji matokeo mazuri kwa sababu anayetukimbiza tumemuacha kwa pointi moja na amekuwa na mfululizo wa matokeo mazuri kwa mechi za hivi karibuni tofauti na sisi,” alisema.

Kuhusu mchezo huo, Taoussi alisema timu inaendelea kujiweka tayari na matarajio ni kukusanya pointi zote zilizobaki.

“Sio rahisi lakini juhudi na kutumia vizuri kila nafasi tutakazozipata ndio itakuwa siri ya mafanikio kwetu. Tunawaheshimu wapinzani wetu, tunatambua wanachanga karata zao ili wabaki Ligi Kuu lakini na sisi tuna malengo yetu.”

Kocha wa Singida BS, David Ouma alisema kwao msimu ndio unaanza kwa sababu wana nafasi mbili muhimu za kuandika rekodi ya kutwaa Kombe la Shirikisho pia kupambania nafasi ya tatu ambayo wanamuombea mpinzani adondoshe pointi.

“Timu ipo kwenye morali wachezaji wanalitaka taji na nafasi ya tatu ili iwe maandalizi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.”