Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kijili ataja kinachombeba SBS

Dar es Salaam. Beki Kelvin Kijii anayecheza katika kikosi cha Singida Big Stars (SBS) ameweka wazi kwamba sababu kubwa inayomfanya awe kwenye kiwango cha juu ni kutokana na ushindani wa namba uliopo baina yake na wenzake.

Kijili amejiunga na Singida BS msimu huu baada akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na kikosi cha KMC.

Kijili alisema kuna changamoto kubwa ya namba kwa sababu wachezaji wote ni wazuri wanaocheza nafasi yake hivyo inamuhamasisha kujituma zaidi.

"Najisikia vizuri sana kuwa kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu ushindani ambao upo ni mkubwa sana, juhudi zangu ni kutokana na ushindani wa hapa;

"Nafanya sana mazoezi, binafsi na timu, pamoja na kujitunza hiyo ndio siri kubwa ya kiwango changu mimi kuhakikisha nakuwa bora,"

Kijiri katika nafasi yake anachuana na wachezaji kutoka nje ya nchi, Nico Wadada (Uganda) na Nicolas  Gyan (Ghana) lakini wote wanasubili dhidi yake.

Beki huyo amekuwa na kiwango kizuri tangu msimu uliopita akiwa na KMC hali ambayo imewafanya mabosi wa Singida BS wamsajili msimu huu.