Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kichuya apiga bao

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Shiza Kichuya 

Muktasari:

Kichuya ametwaa tuzo hiyo sambamba na kujinyakulia kitita cha Sh.1 Milioni kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Kampuni ya Vodacom akiwapiga bao nyota wenye majina kama, Ibrahim Ajib wa Simba na Donald Ngoma wa Yanga.

KIUNGO Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Shiza Kichuya amewafunika kina Donald Ngoma wa Yanga na Ibrahim Ajib akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi uliopita wa Machi, huku akisema hiyo imempa mzuka zaidi.

Kichuya ametwaa tuzo hiyo sambamba na kujinyakulia kitita cha Sh.1 Milioni kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Kampuni ya Vodacom akiwapiga bao nyota wenye majina kama, Ibrahim Ajib wa Simba na Donald Ngoma wa Yanga.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kichuya alisema alishawahi kujiuliza maswali lini atakuwa mchezaji bora kama ilivyotokea kwa wenzake na sasa anashukuru kwa sababu sehemu ya malengo yake yamekamilika.

“Kuna siku niliwaza jambo hili na nilijijibu natakiwa kupambana, na wewe unanipigia simu unaniambia hivi, kumbe imetimia, nashukuru kwani sehemu ya ndoto zangu zimeanza kufanikiwa na hata hivyo sitabweteka, nitapambana zaidi ili nitwae zawadi nyingine nyingi kama hizi,” alisema Kichuya ambaye anaichezea pia timu ya taifa.

Katika tuzo hiyo ya Machi, Kichuya alichuana na Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar, na Abdulrahman Mussa wa JKT Ruvu Stars.

Mbali na Kichuya wengine waliotwaa tuzo hiyo kwa miezi ya nyuma ni Mzimbabwe wa Yanga, Thaban Kamusoko (Desemba 2015), kiraka wa Azam, Shomari Kapombe (Januari 2016) na Mohamed Mkopi wa Prisons (Februari 2016).

Wakati huo huo, TFF imelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa soka kufanya vurugu katika mechi ya Simba na Toto Africans Uwanja wa Taifa, mchezo ambao Wekundu wa Msimbazi walichapwa bao 1-0.

TFF imewaasa, wanachama na mashabiki kuwaheshimu viongozi wa klabu zao waliopo madarakani na kusisitiza kama kuna tofauti wakajadiliane klabuni kwao na siyo kama walivyofanya mashabiki wa Simba kwa kuanzisha vurugu uwanjani hapo.