Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibu: Yanga wana motoo, afunguka ishu nzima!

Muktasari:

STRAIKA gumzo kwa sasa kwenye Ligi Kuu ya Bara, Kibu Denis amesisitiza kwamba Yanga wana moto sana wa kupata saini yake.

STRAIKA gumzo kwa sasa kwenye Ligi Kuu ya Bara, Kibu Denis amesisitiza kwamba Yanga wana moto sana wa kupata saini yake.

Staa huyo wa Mbeya City anawindwa pia na Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Kibu ameliambia Mwanaspoti kwamba alifanya mazungumzo na viongozi wa timu zote mbili akiwa na msimamizi wake aliweka mahitaji yake na ambao watakuwa tayari kumpatia ndio anaweza kusaini lakini akakiri kwamba Yanga ndio wana kasi sana.

Alisema ukiachana na ofa za timu hizo mbili kuna wengine ambao nao kwa nyakati tofauti wamemuulizia jinsi ya kumpata na kama wataweza kufika pale ambapo anahitaji katika maslahi yupo tayari.

“Unajua mpira ndio kazi yangu ni ngumu kueleza naweza kwenda kucheza katika timu gani msimu ujao kwani ambacho nahitaji kwanza wakati huu ni kuweka alama hapa Mbeya City ili hata nikiondoka niweze kukumbukwa,” alisema Kibu.

“Katika timu hizi mbili kubwa nchini Yanga wameonekana kuwa mstari wa mbele katika mazungumzo nami kwani katika nyakati tofauti wamewasaliana sana na msimamizi wangu.

“Si muda mrefu mara baada ya kumaliza msimu nitatoa msimamo wangu kuwa nibaki hapa Mbeya au msimu ujao nitaenda katika moja ya hizo timu kubwa au nyingine yoyote,” aliongeza.

Kibu amekuwa na kiwango bora msimu katika kikosi cha Mbeya na hata alipocheza mara ya kwanza Taifa Stars dhidi ya Malawi alionyesha kiwango bora licha ya kutokea benchi.

Jambo hilo limewavutia wakongwe Yanga na Simba kuhitaji huduma yake kwa ajili ya msimu ujao pamoja na timu nyingine ambazo mwenyewe hakutaka kuziweka wazi.

Katika hatua nyingine kocha wa Simba, Didier Gomes alisema, Kibu ni kati ya wachezaji wa Mbeya City wenye uwezo wa kutimiza majukumu sahihi uwanjani.

Gomes alisema katika wakati tofauti amemfuatilia Kibu na kubaini ni mchezaji mzuri mzawa waliopo ligi msimu huu kwani anaweza kuwasumbua mabeki na kufunga mwenyewe.

“Kama akipata nafasi ya kucheza zaidi ni moja ya wachezaji wazuri, kocha yeyote mpinzani ambaye anakutana nae lazima ataweka mipango ya kumzuia kama ilivyokuwa kwangu,” alisema Gomes.