Kazi ipo kwa Mwendwa

Mwendwa akamatwa tena

RAIS wa Shirikisho la Soka (FKF), Nick Mwendwa, ambaye aliondolewa ofisini hivi karibuni, amekamatwa tena.

Mwendwa, alikamatwa jana jioni na kupelekwa katika ofisi za makao makuu ya idara ya upelelezi wa makosa Jinai (DCI), iliyoko maeneo ya Kiambu Road.

Akizungumzia kukamatwa kwa bosi wake, Mkurugenzi wa mtendaji wa FKF, Barry Otieno, bosi huyo wa shirikisho hilo, lililovunjiliwa mbali hivi karibuni kutokana na tuhuma za matumizi ya fedha za umma, alikamatwa jana saa 6:30 mchana, maeneo ya Kiambu Road.

Kwa mujibu wa barua ya Mawakili wa Mwendwa, iliyosainiwa na Wakili Eric Mutua, kwenda kwa Mkurugenzi wa DCI, Mwendwa alikuwa njiani kwenda katikati ya Jiji, akitokea Runda, gari lake liliposimamishwa na makachero hao, ambao walimkamata na kumpeleka makao makuu ya DCI.

“Ni kweli mteja wetu amekamatwa. Alikuwa njiani, maeneo ya Kiambu Road, akitokea Runda kuelekea Jijini, gari lake liliposimamishwa na gari nyingine, wakashuka makachero wawili, ambao walimkamata na kumpelekea makao makuu ya DCI,” ilisema barua hiyo.

Mwendwa, alikuwa ameachiwa huru Alhamisi, baada ya upande wa mashtaka (Jamhuri) kuamua kufunga faili lake, kufuatia amri ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya Milimani, Wandia Nyamu, aliyewaamuru kuandaa mashitaka yenye mashiko dhidi ya Mwendwa ama aachiwe huru.

Baada ya kuachiwa Barry alijishasha afisi yao bado ndio iko mamlakani.

Mwendwa alikamatwa na kutupwa jela kabla ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa na ubadhirifu wa fedha za serikali zaidi ya Sh200 milioni.

Baada ya kufikishwa mahakamani wiki iliyopita, serikali ilishtumiwa kwa kushindwa kuwasilisha kesi kisawasawa na kupewa siku saba kuandaa mashtaka mapya kabla ya kuachiwa huru na kutaka kurejea uongozini na Alhamisi na Mwendwa alikamatwa tena.