Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaze, Mkude wanukia Singida Big Stars

Muktasari:

  • Wakati kocha wa Singida Big Stars, Hans Pluijm akitajwa kupewa mkono wa kwaheri, kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze ndiye anatajwa anaweza kurithi mikoba yake.

TETESI ZA USAJILI

KAZE - Wakati kocha wa Singida Big Stars, Hans Pluijm akitajwa kupewa mkono wa kwaheri, kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze ndiye anatajwa anaweza kurithi mikoba yake.


MKUDE - Kiungo mkongwe aliyeichezea Simba kwa miaka 11, Jonas Mkude huenda akajiunga na Singida Big Stars ama kubaki Msimbazi kutokana na mvutano wa viongozi uliopo kwa sasa.

KAMETA - Beki wa pembeni, David Kameta 'Duchu' anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Azam FC msimu ujao, wakati miamba hiyo ya Chamazi ikiwa 'bize' na kusafisha timu kwa ajili ya usajili mpya.

BRYSON - Tangu beki wa kushoto, David Byrson, ajiunge na Yanga 2021, hakuwahi kucheza kwa kiwango kikubwa, hivyo inasemekana ni kati ya wachezaji ambao panga linawahusu na huenda akarejea kwenye timu yake ya zamani, KMC.

MASEKE - Kipa aliyeachwa na Azam FC, Wibol Maseke huenda akwa sehemu ya kikosi cha KMC ama Geita Gold msimu ujao, kutokana na timu hizo kuonyesha nia ya kumsajili.