Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaze amuanzisha Kibada Yanga ikipasha silaha

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Yanga inakutana na African Sports ya Tanga katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu ambapo pia mshambuliaji wao mpya Fiston Abdulrazack akianza katika mchezo wake wa kwanza tangu asajiliwe.

Yanga imetoa kikosi chake kinachoshuka uwanjani dakika chache kutoka sasa ikiwakaribisha African Sports ya Tanga.

Katika mchezo huo wa kirafiki ambao Yanga inataka kuutumia kurudisha ufiti wa mechi kocha mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze amemuanzisha mshambuliaji wake mpya raia wa Burundi Fiston Abdulrazack.

Huu unakuwa mchezo wa kwanza was Fiston tangu asajiliwe na Yanga katika dirisha dogo la usajili huku beki wao mpya Dickson Job akikosekana kabisa sababu ikitajwa ni majeruhi.

Katika safi ya ulinzi Kaze ameanza na kipa Mkenya Farouk Shikhalo aliyefanya vyema katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi akifanya vyema na kuipa Kombe hilo timu hiyo.

Mabeki Paul Godfrey "Boxer' akianza upande wa Julia,kushoto akianza Adeyun Saleh wakati mabeki wa kati wakiwa Lamine Moro akianza na Mukoko Tonombe.

Katika kiungo Yanga itaanza na Zawadi Mauya,Omar Chibada,Haruna Niyonzima na Tuisila Kisinda.

Safu ushambuliaji Yanga itaanza na Waziri Junior na Fiston ambaye macho ya mashabiki wengi wa Yanga watakuwa wakimtazama yeye kujua ubora wake.

Katika benchi Kaze amewapa nafasi kipa Metacha Mnata,Said Juma,Mustapha Yassin,Deuse Kaseke,Farid Mussa,Feisal Salum,Ditram Nchimbi na Carlos Guimaraes 'Carlinhos'.