Kaze abadili mbinu za kuivaa Mtibwa

Saturday February 20 2021
kazee pic
By Waandishi Wetu

Dar es Salaam. Jeshi la kocha Cedrik Kaze linashuka uwanjani leo kuivaa Mtibwa Sugar kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kaze ameiongoza Yanga katika michezo mitatu ya Ligi Kuu bila ushindi, akianza na sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, sare kama hiyo dhidi ya Mbeya City na na 3-3 dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mchezo uliopita, kocha huyo alilazimika kumwingiza Mukoko Tonombe ili kuinusuru Yanga, ambayo ilishakuwa nyuma kwa mabao 3-2.

Lakini katika mchezo waleo, kiungo huyo raia wa DR Congo anaweza kukosekana kutokana na kushindwa kufanya maz-oezi ya mwisho na kikosi hicho, jana asubuhi.

Licha ya kukosekana kwa kiungo huyo, kocha Kaze alimtumia Said Makapu kama mbadala wa Tonombe na mchezaji huyo alionyesha kumudu vyema nafasi hiyo akicheza sambamba na kiungo Feisal Salum.

Pia, winga machachari ambaye hutumia spidi kupeleka mashambulizi kwa wapinzani, Yacouba Sogne ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha, naye alikuwa sehemu ya kikosi.

Advertisement

 Katika mazoezi hayo, Kaze alian-za kwa kumjumuisha mshambuliaji wake mpya, Fiston Abdulrazack kati-ka kikosi cha akiba kisha alimuweka katika kikosi cha kwanza.Mchezaji huyo ambaye alikuwepo katika mchezo dhidi ya Mbeya City alikosekana kabisa katika kikosi kilichocheza dhidi ya Kagera Sugar na sasa amerejeshwa.


Saido aanza mazoezi

Mshambuliaji Saido Ntibazonkiza, ambaye ilielezwa kwamba anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja na atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne, ameonekana jana mazoezini.

Hizo zitakuwa habari njema kwa mashabiki wa Yanga, ambao wanahisi kumkosa nyota huyo wa kimataifa wa Burundi, ambaye alianza kwa mabao mawili na pasi tatu za mabao katika kikosi cha miamba hiyo.

Mwanaspoti  lilimshuhudia Saido akifanya mazoezi yote tangu kikosi hiko kikianza mazoezi saa 4:30 asubuhi hadi saa 5:43 asubuhi.


 Yanga waishukia TFF


Uongozi wa Yanga umeishutumu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tan-zania (TFF) na mamlaka zake zote ukidai hawaiten-dei haki timu yao.

Akizungumza jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema katika michezo yao miwili iliyo-pita kumekuwa na uamuzi tata mara kadhaa, jambo wanalodhani linafanywa kuwamiza kwa makusudi.

yanga pic mwakalebela

Mwakalebela alisema katika mchezo wao wa Mbeya City walinyimwa penati mbili za wazi ambazo walistaili kuzipata na zingepelekea wao kushinda mchezo huo na sio kupata pointi moja.

Alisema mbali na mchezo huo hata mchezo na Kagera nao walinyimwa penalti, ambazo zingewafanya kupata pointi tatu badala ya kupata moja, huku akikiri kuamini mamlaka hizo kuna timu inayoandaliwa kuwa bingwa.

“Sisi kama Yanga tumewakosea nini mpaka mnatufanyia hivi, au hatustaili kucheza ligi ya Tanzania tujue, hivi vitu vinavyofanyika uwan-jani vinawafanya hata mashabiki kukosa uvu-mulivu,” aliongeza.

Advertisement