Katwila aipa tahadhari Mtibwa Sugar

Muktasari:
- Mwalwisi aliyejiunga na kikosi hicho akitoka TMA FC ya jijini Arusha aliyoiongoza katika michezo 15 ya raundi ya kwanza, alisema sare hiyo nyumbani imeharibu mipango yao, hivyo kilichobakia ni miujiza kutoka kwa wapinzani wao waliokuwa juu.
ALIYEKUWA Kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila ameipongeza timu hiyo kwa kurejea tena Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wa 2025-2026, huku akiwataka viongozi wa kikosi hicho kwa sasa kuhakikisha hawarudii makosa, yaliyowafanya kushuka daraja.
Katwila ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Bigman FC, ametoa kauli hiyo baada ya sare ya kikosi hicho ya bao 1-1, dhidi ya Mtibwa Sugar, iliyoipa nafasi ya kurejea tena Ligi Kuu Bara, baada ya kufikisha pointi 67 katika michezo 28, iliyocheza.
“Nawapongeza sana kwa juhudi kubwa ambazo wamezionyesha kwa sababu Ligi ya Championship sio rahisi kama wengi wetu ambao tunafahamu, naamini siri iliyowasaidia ni kubaki na wachezaji wazoefu ambao wamesaidia kufika walipo,” alisema Katwila.
Katwila ni kocha aliyeishusha daraja Mtibwa Sugar msimu uliopita.