Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karibu tena Maximo changamoto zilezile

MAXIMO Pict

Muktasari:

  • Baada ya kuja mara ya kwanza kuinoa timu ya taifa, Taifa Stars na baadaye mara ya pili akaja kuifundisha Yanga, Maximo sasa anakuja kufanya kazi katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano, yaani visiwa vya Zanzibar.

KIJIWE kimepata taarifa za uhakika kuwa, kuna uwezekano mkubwa aliyekuwa kocha kipenzi cha Watanzania Marcio Maximo akarejea nchini.

Baada ya kuja mara ya kwanza kuinoa timu ya taifa, Taifa Stars na baadaye mara ya pili akaja kuifundisha Yanga, Maximo sasa anakuja kufanya kazi katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano, yaani visiwa vya Zanzibar.

Maximo atakuja kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes lakini wakati huo akifanya jukumu jingine la kuendeleza vipaji vya soka katika visiwa vya Pemba na Unguja.

Majukumu yote hayo mawili yanaweza kutimizwa kwa ufasaha kabisa na Maximo akibebwa na uzoefu alionao wa takribani miaka minne wa soka la Tanzania akifundisha katika ngazi ya timu ya taifa na klabu.

Na Zanzibar ni sehemu ambayo Maximo atapata raha sana maana vipaji vipo tena vya kutosha na vingi vina umri mdogo kwa vile kule wanathamini sana soka la vijana na watoto wanafundishwa misingi sahihi ya kucheza soka mapema.

Bahati mbaya ya Maximo ni kwamba atakutana na changamoto zilezile ambazo alizikuta wakati ule alipokuja kuikochi Taifa Stars na hata kipindi  ambacho aliinoa Yanga na ya kwanza ni Zanzibar Heroes kutokuwa na wigo mkubwa wa mashindano.

Mashindano pekee ambayo Zanzibar Heroes inayategemea ni Kombe la CECAFA ambayo nayo kwa muda mrefu yamekuwa hayafanyiki na mara ya mwisho yalichezwa Uganda mwaka 2019, hivyo Maximo hatopata jukwaa la kuonyesha kile ambacho atakifundisha.

Changamoto nyingine ni kwamba kocha wa Zanzibar Heroes hana nguvu wala mamlaka yoyote makubwa katika timu ya taifa ya Taifa Stars, hivyo Maximo hata azalishe vipaji vingi kiasi gani, bado kutumika kwao timu ya taifa kutategemea utashi wa kocha wa Taifa Stars kipindi hicho.

Kwa hadhi ya Maximo ilitakiwa Zanzibar Heroes iwe inashiriki mashindano mengi tofauti ili tujiridhishe kama alistahili kukaa kwa muda mrefu alipokuja nyuma au uamuzi ambao ulichukuliwa juu yake kipindi hicho ulikuwa sahihi.