Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapombe amaliza ubishi Simba

BEKI mahiri wa Simba, Shomari Kapombe amemaliza ubishi Msimbazi kwa kuwataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi katika mataji yote ambayo yako usoni kwao, kwani wanajua nini wanakifanya na kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Kapombe, anayemudu zaidi ya nafasi moja uwanjani na mmoja wa mabeki wa kulia walio bora kwa sasa alisema kama wachezaji, wanajua jukumu lao ni moja tu la kusakata kabumbu na kuwapa burudani mashabiki wao waliokuwa sehemu kubwa ya wao kupata mafanikio ndani ya dakika 90.

Hivyo, akawaka wasiwaze sana juu ya kasi ya wapinzani wao kwenye Ligi Kuu, kwani anauhakika watalitetea tena taji hilo kwa mara ya nne mfululizo kwa madai uwezo huo wanao.

Simba pia ina kazi ya kutetea Kombe la ASFC ililotwaa msimu uliopita kwa kuinyoa Namungo.

“Wachezaji tunapambana na kutimiza wajibu wetu uwanjani, hivyo wanasimba wote ni wakati wao wa kutamba juu ya mataji tutahakikisha tunapambana,” alisema Kapombe.

Aidha, alisema, hata katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikitinga makundi wamepania kupigana ili kufika mbali zaidi kuliko misimu miwili iliyopita walipokwamia robo fainali.

“Tulianza katika hatua ya mtoano na sasa tumefanikiwa kuingia makundi, ni mipango ya Mungu na juhudi zetu sisi kama wachezaji kwa ushirikiano na benchi la ufundi na uongozi bila kusahau mashabiki, tutafika mbali zaidi,”

Pia Kapombe alizungumzia jinsi majeraha yalivyokuwa yakimrejesha nyuma ila kwa sasa anamshukuru Mungu yuko fiti kwa ajili ya kupambani timu yake na ya Taifa pia.

“Majeraha yaliniandama sana ila kwa sasa namshukuru sana Mungu niko vizuri, namuomba Mungu nisiumie tena,” alisema.