Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kalambo aja kivingine Bara

Kalambo Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo amekamilisha dili hilo siku ya mwisho ya dirisha la usajili kufungwa Januari 15, baada ya kuachana na Geita Gold inayoshiriki Ligi ya Championship, huku akieleza malengo yake tangu mwanzoni ya kurejea Ligi Kuu Bara yametimia.

BAADA ya kipa Aaron Kalambo kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Coastal Union, nyota huyo ameweka wazi mojawapo ya malengo yake kipindi hiki cha miezi sita iliyobakia kumaliza msimu, ni kurejesha heshima yake iliyotoweka ghafla.

Nyota huyo amekamilisha dili hilo siku ya mwisho ya dirisha la usajili kufungwa Januari 15, baada ya kuachana na Geita Gold inayoshiriki Ligi ya Championship, huku akieleza malengo yake tangu mwanzoni ya kurejea Ligi Kuu Bara yametimia.

"Jambo kubwa ni kupambana tena kila na nitapata nafasi ya kucheza, natambua ushindani ni mkubwa lakini nimejipanga ipasavyo kuhakikisha narejesha heshima yangu kama ilivyokuwa mwanzoni, nimefuata changamoto mpya na nitaipambania sana."

Kipa huyo wa zamani wa Dodoma Jiji, alisema wakati anaenda Geita Gold alipata ofa ya KenGold inayoshiriki Ligi Kuu Bara ingawa kitendo cha kushindwa kufikia masilahi kilimfanya kushindwa kukitumikia, japo hakukata tamaa akiwa Championship.

"Niliamini ni suala la muda tu kurejea tena Ligi Kuu, unajua unapocheza huku ndio sehemu ya kuonekana na kujiuza zaidi japo hata kwa sasa Championship imekuwa kubwa, nashukuru kwa nafasi hii niliyoipata na nitaipambania kwa hali na mali."

Kalambo anaenda kushindana na kipa, Chuma Ramadhani ambaye amekuwa panga pangua kikosi cha kwanza baada ya kuondoka kwa Mkongomani Ley Matampi, akiungana na mastaa wengine wapya akiwemo mshambuliaji, Amara Bagayoko aliyetoka ASKO de Kara ya Togo.

Wengine ni Raphael Daudi, Mizar Kristom na Ritch Nkoli (Namungo FC), Vitalis Nkosi (Fountain Gate), Sabri Kondo (KVZ), Gustapha Saimon (Dodoma Jiji), Mgaza Hamisi Ally kutokea Falme za Kiarabu na Fales Gama kutoka Yanga chini ya miaka 20.