Kahama Sixers yaivuruga Veta

Muktasari:
- Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Veta, katika mchezo wa kwanza kwa timu hiyo, Kahama Sixers iliishinda Risasi kwa pointi 54-46.
TIMU ya mpira wa kikapu ya Kahama Sixers imedhihirisha ubora ilionayo katika Ligi ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kuiadhibu Veta kwa pointi 75-37.
Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Veta, katika mchezo wa kwanza kwa timu hiyo, Kahama Sixers iliishinda Risasi kwa pointi 54-46.
Katika mchezo huo, Julius George wa timu ya Kahama Sixers aliongoza kwa kufunga pointi 37, akifuatiwa na Arnold Mushi aliyefunga pointi 12.
Kwa upande wa timu ya Veta alikuwa Jimmy James aliyefunga pointi 11, akifuatiwa na Landry Landry aliyefunga pointi 8.
Katika mchezo mwingine, timu ya Risasi iliishinda B4 Mwadui kwa pointi 75-73, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Risasi.
Katika mchezo huo, Nuhu Makanga wa timu ya Risasi alifunga pointi 24, akifuatiwa na Vicent Mangula aliyefunga pointi 13.
Kwa upande B4 Mwadui alikuwa Benedicto Kafula aliyefunga pointi 21, akifuatiwa na John Loso aliyefunga pointi 20.
Kamishina wa ufundi na mashindano wa Ligi ya kikapu mkoa wa Shinyanga, George Simba, amesema mfumo unaotumika, ni wa kila timu kucheza nyumbani na ugenini.