Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kahama Sixers yaichapa Risasi

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanasposti kwa simu kutoka Shinyanga, kamishina wa ufundi na mashindano wa mkoa huo, George Simba alisema timu nne ndizo zinazoshiriki michuano hiyo.

Timu ya kikapu ya Kahama Sixers imeifunga Risasi kwa pointi 87 -64 katika mchezo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Shinyanga uliofanyika  Uwanja wa Kahama.

Akizungumza na Mwanasposti kwa simu kutoka Shinyanga, kamishina wa ufundi na mashindano wa mkoa huo, George Simba alisema timu nne ndizo zinazoshiriki michuano hiyo.

Alizitaja timu hizo kuwa ni Kahama Sixers, Risasi, B4 Mwadui na Veta.

Kwa mujibu wa Simba kila timu itacheza na mwenzake na mshindi wa kwanza atacheza na mshindi wa nne, ilhali yule wa pili na wa tatu watakipiga kwa mfumo wa ‘best of  three pray off’.

Akizungumzia mashindano hayo, nyota wa Risasi, Yohana William alisema kukosekana kwa wachezaji muhimu wa timu yao kulichangia kupoteza mchezo huo.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni John Bayo, Charles Dismas na mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Silas.

Alieleza kuwa changamoto nyingine iliyojitokeza kwenye mchezo huo ni utelezi.

Katika mchezaji huo Kahama Sixers iliwatumia wachezaji wote nyota akiwemo Julias George, Yusuph, Francis William, Anorld na mwingine aliyetajwa kwa jina la Canisius.