Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagera Sugar nne zinawatosha Uganda

Kagera Pict
Kagera Pict

Muktasari:

  • Kagera iliyokuwa kambini tangu Julai 12 kwa ajili ya pre season kwenye Uwanja wa Kaitaba na kisha katika fukwe za Ziwa Victoria mjini humo chini ya Kocha Msaidizi, Marwa Chambeli na kocha wa makipa, Juma Kaseja.

KIKOSI cha Kagera Sugar kimeondoka leo Alhamisi kutoka Bukoba kwenda Uganda kunoa makali ya wachezaji wake kwa kucheza mechi nne za kirafiki ili kujipima nguvu kabla ya kurudi nchini kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho 2024-2025.

Kagera iliyokuwa kambini tangu Julai 12 kwa ajili ya pre season kwenye Uwanja wa Kaitaba na kisha katika fukwe za Ziwa Victoria mjini humo chini ya Kocha Msaidizi, Marwa Chambeli na kocha wa makipa, Juma Kaseja.

Akizungumzia safari hiyo, kocha Chambeli alisema "Tunaenda Kampala, kwa ajili ya maandalizi ya mwisho na kucheza mechi za kirafiki, tunatarajia kucheza tatu hadi nne. Timu zipo tukifika tutapata mrejesho ni zipi, pia tunatarajia kukaa huko kwa siku tano mpaka sita."

Kabla ya kuanza safari hiyo, wiki hii timu hiyo imeshiriki matukio mbalimbali ya kijamii, Agosti 4 kikosi na benchi la ufundi kilitembelea msitu wa asili wa Rubare na kufanya utalii wa ndani na Agosti 6 wachezaji na benchi la ufundi walipewa darasa kusisitiza malengo ya timu na wajibu wa kila mmmoja kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

Ikiongozwa na Mtendaji Mkuu mpya, Thabiti Kandoro, juzi (Jumatano), Kagera Sugar ilishiriki shughuli za kijamii kwa kutembelea na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kituo cha yatima cha Nusuru Yatima Association kilichopo Kashai mjini Bukoba na Julai 26, CEO huyo alikutana na kuzungumza na wazee na wadau wa soka mkoani Kagera.

Akizungumzia ushiriki wa matukio hayo ya kijamii, Kandoro alisema ni sehemu ya kuiweka karibu timu na wananchi wa Kagera ili kupata ushirikiano wao na kuisaidia kufanya vizuri Ligi Kuu, huku pia wakituma ujumbe kwa jamii na kuwa kinara wa kutangaza vivutio vya utalii, kuhifadhi na kutunza mazingira.

"Msimu huu sisi hatutacheza ligi peke yake tutacheza tukiwa na ujumbe kwa jamii yetu kuhakikisha mpira wetu unafikisha ujumbe kwa hadhira, yapo mambo ambayo bado tunaangalia jinsi gani ya kuyabeba kuyapeleka kwa jamii kama timu mojawapo ni mazingira tushawishi wananchi na kuwa mabalozi," alisema Kandoro.