Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Evalisto aendelea kusubiri ofa mpya

EVARISTO Pict

Muktasari:

  • Evalisto alimaliza mkataba wa miezi sita na Makadi FC mwezi Machi mwaka huu, akiwa ametokea Mlandege FC ya Zanzibar.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Makadi FC ya Misri, Oscar Evalisto amesema bado hajasaini mkataba mpya kwenye klabu hiyo, akisubiri ofa kutoka timu nyingine.

Evalisto alimaliza mkataba wa miezi sita na Makadi FC mwezi Machi mwaka huu, akiwa ametokea Mlandege FC ya Zanzibar.

Akizungumza na Mwanaspoti, Evalisto alisema bado anaendelea na mazungumzo na timu mbalimbali kutoka Tanzania na Misri.

“Kuna timu nafanya nazo makubaliano hapa Bongo, lakini pia Misri wanataka nirudi. Tukifikia mwafaka mzuri, naweza kurudi. Hivyo hivyo pia naweza kubaki Bongo nikipata klabu yenye ofa nzuri,” alisema nyota huyo.

Aliongeza kuwa kucheza ligi ya Misri kumempa uzoefu mkubwa, hasa baada ya kucheza Ligi Kuu ya Zanzibar akiwa na Mlandege na timu za vijana kama Lipuli FC.

“Misri nimekutana na wachezaji wenye uzoefu na CV kubwa. Hilo limenijenga na kunikomaza. Naamini kama nitaendelea kuwepo, nitaongeza vitu zaidi kwenye soka langu.”

Mshambuliaji huyo alisajiliwa kwenye dirisha dogo, alicheza mechi tatu na kufunga mabao mawili.