Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kadi ya Banda ina mambo mengi ndani yake

Muktasari:

Mchezo haukwenda dakika 90 kama ilivyotabiriwa na wengi. Ndani ya dakika hiyo ya 24, Abdi Banda alipewa kadi nyekundu. Kwa Yanga hii, unapopungua halafu ndani ya dakika hizo, ni wazi kwamba mpira unakuwa umekwisha. 


MPIRA uliokuwa unasubiriwa kwa hamu huku Yanga ikiwa imejificha Pemba kwa majigambo na chembe chembe za hofu na huku Simba ikiwa imejificha Morogoro kwa majigambo na chembe chembe za hofu, ulimalizika dakika ya 24 tu ya mchezo.

Mchezo haukwenda dakika 90 kama ilivyotabiriwa na wengi. Ndani ya dakika hiyo ya 24, Abdi Banda alipewa kadi nyekundu. Kwa Yanga hii, unapopungua halafu ndani ya dakika hizo, ni wazi kwamba mpira unakuwa umekwisha. 

Wachezaji wa Simba walifahamu hivyo na morali ikapotea. Mashabiki wa Simba walifahamu hivyo na morali ikapotea. Hata mabosi wa Simba waliokuwa jukwaa kuu walifahamu hivyo na morali ikapotea. Nilichukia kuona hali hiyo. Mwamuzi alikuwa amelimaliza pambano mapema. Pambano ambalo lilipaswa kuwa kali huku wanaume 22 wakipambana uwanjani.

Kadi ya Banda ina mambo mengi ndani yake. Kwanza kabisa tuache kumjadili mwamuzi Jonesia Rukyaa. Tuanze na kocha wa Simba, Jackson Mayanja. Nilianza kumuona akimtumia Banda kama beki wa katika mechi za Simba Kanda ya ziwa. Banda ni beki asiye na kasi. Alipokuwa Coastal Union alikuwa beki wa kushoto. Simba ilimsajili kama mchezaji wa nafasi hiyo. Baada ya muda Simba walimuhamishia nafasi ya kiungo kwa kuhofia kuwa kushoto alikuwa hana kasi.Na sasa wamemrudisha kama beki wa kati. Ni kitu kinachostaajabisha. Nilifahamu mapema na nikaongea katika Kituo cha Televisheni cha Azam TV kwamba Banda angepata matatizo kwa kasi ya Donald Ngoma na Simon Msuva kama ingetokea akikabiliana na watu hao.

Dakika za mwanzo tu alipewa kadi ya njano, kwa kumvuta chini Ngoma upande wa Magharibi mwa uwanja. Kwa mchezaji kama yeye asiye na kasi halafu anacheza kama mtu wa mwisho alikuwa anatembea katika mstari mwembamba kuweza kumaliza mechi bila ya kadi nyingine ya njano.Hatimaye likaja tukio ambalo lilimtia matatani. Ni kweli Banda alihisi kwamba asingeweza kukabiliana na kasi ya Ngoma akaamua kumsukuma katika njia yake bila ya kutazama mpira. Ilikuwa ni faulo. Hakuna ubishi kwa hilo. Swali ni je, ilistahili kadi ya pili ya njano iliyoharibu mpira wote au hapana?

Katika macho ya awali nilimlaumu Mwamuzi. Alikuwa anatuvurugia mechi tamu tuliyoisubiri kwa hamu. Nilidhani kwamba alichopaswa kufanya Jonesia ni kumuita Banda na kumwambia kuwa angecheza tena faulo angemtoa nje kwa kadi nyekundu.

Banda hakuwa amefanya faulo ya kudhuru mwili. Nilidhani mwamuzi alipaswa kuulinda mchezo. Ni kitu cha kawaida katika mechi kubwa ambazo zinasubiriwa kwa presha kubwa. Sio kila faulo ya pili ya mchezaji aliyepewa kadi ya njano, basi inapaswa kuwa kadi ya pili ya njano. Mchezaji mwenye kadi moja ya njano uwanjani hapaswi kuwa mfungwa. 

Hata hivyo, Jonesia aliamua kutumia kanuni inayompa nguvu zaidi. Aliangalia zaidi kuwa Banda alikuwa katika mstari wa mwisho na Ngoma angeweza kufunga. Waingereza na wenye Lugha ya Kiingereza wanasema ‘Scoring Opportunity’.

Hiyo ndio kanuni ambayo Jonesia aliitumia na naweza kukubali. Ndio kanuni ambayo aliitumia kutunyima uhondo katika mechi ya juzi. Ndio kanuni ambayo ilisababisha Yanga ishinde kilaini katika mechi ambayo timu zote mbili zilikutana zikiwa ziko vizuri. Kwa kanuni hii ilikuwa kadi nyekundu halali kabisa na sina matatizo nayo.

Ni kanuni hii hii imekuwa ikitunyima uhondo katika mechi nyingi kubwa duniani ambazo tumezisubiri kwa muda mrefu. Katika siku za karibuni ilitunyima uhondo katika pambano la Arsenal dhidi ya Chelsea lililopigwa Emirates. Per Metersacker akiwa beki wa kati ambaye hana kasi kama ilivyo Banda alimchezea rafu Diego Costa dakika za mwanzo za mechi hiyo na mwamuzi akampa kadi nyekundu ya moja kwa moja. Ni kwa sababu Costa alikuwa anaenda kutazamana na Petr Cech.

Kama Jonesia hakutumia kanuni hiyo katika kumpa kadi ya pili ya njano Banda isipokuwa alikuwa anaamini kuwa Banda alikuwa amecheza faulo mbaya inayostahili kadi, basi alikuwa amekosea sana. Hasa kwa kuamini shinikizo alilokuwa amepewa na wachezaji wa Yanga kabla ya kuonyesha kadi hiyo.

Vinginevyo Jonesia ameonyesha mapungufu makubwa katika mechi hiyo kwa baadhi ya matukio mengine yaliyoendelea uwanjani.  Baadhi ya matukio ambayo hakutoa kadi ni rafu mbaya ya Hassan Kessy kwa Haruna Niyonzima. Hata kama angetoa kadi nyekundu nisingeshangaa sana. Halafu kuna rafu ya Juma Abdul kwa Mwinyi Kazimoto. Na vipi kuhusu Juma Abdul kumsukuma usoni Hassan Kessy mbele ya mwamuzi? Na unashangaa anapopiga filimbi ya faulo baada ya kipa wa Yanga Ally Mustapha Barthez kumvamia mchezaji wake wakati akiokoa kona.