Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jay Msangi afungukia ishu ya Ibrahim Class

Promota wa ngumi za kulipwa nchini ,Jay Msangi wa kwanza kulia akiwa uwanja wa ndege na bondia Ibrahim Class

Muktasari:

  • Akizungumzia ishu ya kumwekea Class dawa kwenye maji , Msangi alisema: “Kama ni kweli nimefanya, basi nitakuwa ‘mafia’ maana katika maisha yangu ya ngumi, sijawahi kusikia tukio kama hilo, tangu enzi za kina Muhamad Ali.”

PROMOTA maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Jay Msangi amejibu tuhuma za kumwekea dawa za kulevya bondia Ibrahim Class na kumtapeli fedha ya malipo ya pambano lililofanyika Afrika Kusini.

Ishu yenyewe ilikuwa hivi. Class alimtuhumu Msangi kumdhulumu fedha za pambano la kuwania ubingwa wa IBF lililofanyika wiki mbili zilizopita.

Bingwa huyo wa zamani wa Dunia wa Global Boxing Council (GBC) alidai aliwekewa dawa za kulevya kwenye maji baada ya kumalizika raundi ya nne ya pambano la raundi 12, huku akimtuhumu Msangi, kitendo kilichosababisha apoteze pambano hilo kwa Technical Knock Out (TKO) raundi ya sita.

Sasa jana Jumapili, promota huyo alikiri kugoma kumpa Class fedha ya pambano, lakini alitaka alipwe kwanza fedha yake ya uwakala Dola 1,800.

“Yote hayo yalitokea baada ya Palasa (Chaurembo) kuwaleta hotelini ‘wahuni’ ili wanifanyie vurugu akidai nimewatapeli fedha zao,” alisema Msangi huku Palasa akikanusha na kudai Msangi alidai alipewa Dola 7,000 badala ya 10,000 hivyo kuhisi dalili za kutapeliwa.

Akizungumzia ishu ya kumwekea Class dawa kwenye maji , Msangi alisema: “Kama ni kweli nimefanya, basi nitakuwa ‘mafia’ maana katika maisha yangu ya ngumi, sijawahi kusikia tukio kama hilo, tangu enzi za kina Muhamad Ali.”

“Nitakuwa wa kwanza duniani, Class alipigwa ngumi ya pua raundi ya pili akalala chini, alihesabiwa hadi saba hakutaka hata kuamka, tulimlazimisha akaamka na kuendelea, lakini hakuwa fiti, alipigwa.”

Pia, Msangi alikiri malipo ya Class yaliibua zogo kwenye hoteli kwani kwenye Dola 10,000, yeye alipaswa kulipwa Dola 1,800 za uwakala, lakini Palasa alimshawishi Class wasimpe baada ya kutokea Watanzania wanaoishi Afrika Kusini aliodai waliletwa na Palasa kuanzisha vurugu.

“Walinifanyia vurugu wakanisachi na kuchukua kila kitu, waliondoka pamoja na Palasa na Class, waliniacha Afrika Kusini hata nauli ya kurudi Tanzania nimepewa msaada,” alisema Msangi.

Msangi aliwahi kuingia kwenye kashfa ya kushindwa kuwalipa mabondia katika pambano la ubingwa wa dunia kati ya Francis Cheka na Phil Williams alisema mambo ya nyuma yasimhukumu, kwani ulikuwa ni ugeni kwenye ngumi na ameandaa ngumi kati ya Cheka na Ajetovic, Mohamed Matumla na Mthailand, Mfaume Mfaume na Habibu Pengo, mapambano kwa mafanikio.