Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jacob Massawe aamsha mastaa Namungo

MASAWE Pict

Muktasari:

  • Namungo ipo nafasi ya 11 kwa pointi 31 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, ambapo imebakiza mechi mbili dhidi ya KenGold na Kagera Sugar kuhitimisha msimu huu, huku ikikabiliwa na upinzani kukwepa play off.

NAHODHA wa Namungo, Jacob Masawe amesema licha ya kukutana na timu zilizoshuka daraja, lakini hawatadharau mechi hizo kutokana na upinzani wa timu zilizo chini yao, huku akishangazwa na historia ya alipotoka timu kupotea.

Namungo ipo nafasi ya 11 kwa pointi 31 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, ambapo imebakiza mechi mbili dhidi ya KenGold na Kagera Sugar kuhitimisha msimu huu, huku ikikabiliwa na upinzani kukwepa play off.

Timu zilizo chini yake ni Pamba Jiji yenye pointi 30 sawa na Tanzania Prisons na Fountain Gate iliyovuna 29, zote zimebakiwa na mechi mbili.

Massawe ambaye amekuwa na baraka za uongozi kutokana na kuvaa kitambaa cha unahodha anapopita, lakini rekodi inaonesha timu alizopita baadhi zimepoteana kwenye medani za soka.

Timu hizo ni Toto Africans ambayo kwa sasa inashiriki ligi ya Wilaya ya Nyamagana (Mwanza), African Lyon (Ligi ya Mkoa), JKT Oljoro iliyouzwa kuwa Gwambina ambayo imepoteana, Ndanda, Stand United na sasa Namungo.

Alisema kwa kipindi hiki cha mapumziko licha ya kutuliza akili, lakini mawasiliano na wenzake yanaendelea katika kukumbushana kutojisahau zaidi kwani bado kibarua ni kigumu.

“Tunakutana na KenGold na Kagera Sugar zote nyumbani, tunajua wameshashuka daraja huenda hawana cha kupoteza, lakini kwetu ni jaribio, lazima tuwe makini kwani walio chini yetu ndio kazi ngumu,” alisema Massawe ambaye pia amewahi kuitumikia Stand United ya Shinyanga.