Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Diamond iko hivi

MAMBO ni moto huko kwenye mitandao ya kijamii, ishu nzima ikiwa ni video ya Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ama Baba Tiffah. Unajua nini? Familia ya staa huyo wa Bongo Flava, imeingia kwenye ligi ya vijembe na vichambo vya hapa na pale kisa ikiwa video wimbo wa Iyena.

Video ya wimbo huo unaofanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na vituo vya redio na runinga, umewaibua watu wa karibu wa Diamond kunangana kwenye akaunti zao za Instagram na kudhaniwa labda ni kiki ya kuupaisha wimbo huo na wengine wakiamini ni hali ya mambo yaliyopo ndani ya familia ya supastaa huyo.

Inazungumzwa hivyo ni kutoka na miezi michache iliyopita Diamond kukiri kuwa yeye ni bingwa wa kutafuta kiki mitandaoni, pia anajulikana kwa kuwa na drama zisizoisha.

Diamond alikiri hayo kwenye mkutano aliofanya na waandishi habari katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kujuzwa mambo kadhaa kuhusu sheria mpya ya mitandao. Si unambukuka?

Sasa kwa kitendo cha Diamond kuachia video na wimbo huo wa Iyena, huko mtandaoni kumechafuka hadi wapo baadhi ya watu wakakumbuka kauli yake ya kupenda kiki mtandaoni na inshu ilikuwa hivi:

CHANZO NI HIKI

Video ya wimbo wa Iyena ilivyoachiwa tu, saa chache ilisababisha familia yake kuanza kutuma posti katika akaunti zao za Instagram huku wakiandika vipande vya mashairi ya wimbo huo ambao, video yake imependwa na mpenzi wa zamani na mama wa watoto wawili wa Diamond, Zari ‘The Boss Lady’, huku baadhi ya mashabiki wakifurahia na kudai mashairi hayo yanamlenga mrembo Hamisa Mobetto, ambaye pia amezaa na Diamond.

Familia ya Diamond imeonekana kutumia wimbo wa video hiyo kama kurusha vijembe kwa Hamisa anayedaiwa hatakiwi na familia ya staa huyo, wakidai eti ni mchafu na hajui hata kutandika kitanda.

MAMA NA MWANA

Vijembe vilianza kwa Mama wa Diamond, Bi. Sandra kupitia akaunti yake ya Instagram kuweka picha ya Zari na kuandika ujumbe wa kumsifia zaidi.

“Mama Latiffah mwenye…#IYENA yake mwanamke usafi gaga kulisugua, mume akirudi sharti viatu kumvua… @diamondplatnumz ft @rayvanny,” ameandika Bi. Sandra kwenye mtandao wake huo.

Naye Esma Platnumz amemjibu mama yake kwa kucomment kwenye picha hiyo kwa kuandika, “Heee kwenye usafi sasa, mama Tee nampongeza wallah dada msafi huyu, kwenye mapishi @wemasepetu unanikomeshaga.”

Mbali ya hao wapo ambao wanajiita timu Zari na timu Wema nao wameandika maneno na kuongeza ya kwao huku wakimtaja Hamisa.

Wapo ambo wanaojiita timu Hamisa na kudai kuwa video ya wimbo huo wa Iyena, inadaiwa imefanyika Septemba mwaka jana kabla ya Zari kutoa tamko la kuachana na Diamond, hivyo wanashauri video irudiwe na Hamisa awe video Queen.

UPANDE WA HAMISA

Kwa upande wa Hamisa Mobetto, katika ukurasa wake wa Instagram, hakujibu kitu ila mama yake mzazi, Shufaa aliamua kuandika ujumbe kwa mara ya kwanza, tangu sakata la Hamisa kuzaa na Diamond na baadhi ya watu wakaanza kumshambulia mtandaoni, hadi kufikia sakata la kudaiwa kupigwa na Bi Sandra, mama huyo hakuwahi kuandika kitu.

Mama Hamisa aliibuka katika mtandao wa Instagram, kwa kuandika ujumbe wa kumpa moyo mtoto wake, baada ya kuona anashambuliwa na familia ya Diamond huku wanaojiita timu Zari, Wema na Lulu wakiunga mkono kitendo wanachofanya familia hiyo.

Mama Hamisa aliandika; “My baby after .... endelea kuwa strong mwanangu, hakuna binadamu anayeweza shusha hadhi yako wala kukudhalilisha, sana sana wanajidhalilisha wenyewe. Hawajakuumba wao wala kukuzaa wao na hakuna wanachoweza kukibadilisha katika maisha yako, hiyo ni mipango ya Allah ...”

Kitendo cha kuandika ujumbe huu wa kumpa moyo na nguvu mtoto wake, kimewatia simanzi baadhi ya watu katika mtandao huo na ukizingatia mama huyo hajawahi kuzungumzia wala kuandika kitu kuwajibu watu wanamshambulia yeye na Hamisa.

MSIKIE MAMA MABETTO

Mwanaspoti lilimtafuta maama Mobetto na kuzungumza naye kuhusiana na uamuzi wake huo, ambapo alisema;

“Ni kweli niiliamua kukaa kimya na nitaendelea kukaa kimya, kwa sababu naona na ninafuatilia kila kitu kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii. Naweza kupoteza maisha huku siku zangu zikiwa bado hazijatimia, nimeandika hivyo ili watu wajue Hamisa ana mzazi wake na yuko hai na sio mtoto aliyekosa wazazi hadi ifikie hatua ya kumweka midomoni kila kukicha.

“Embu angalia jana watu walivyoanza kumwandama, Hamisa alizima simu kutwa nzima kwa sababu alikuwa anasumbuliwa kwa kupigiwa simu na meseji nyingi. Amekuja kuwasha jioni kabisa, lakini bado simu zilikuwa zinaendelea kuingia, ila mie nasema tu Mungu ni wetu sote.”

HARMONIZE NAYE

Sasa kama ulidhani picha liliishia hapo, basi utakuwa umekosea sana. Mambo yalihamia kwa Hamornize. Baada ya yote hayo, mida ya usiku ishu nzima ilihamia kwa msanii huyo wa WCB, Harmonize kwa kuposti picha ya Hamisa Mobetto na kuandika ujumbe katika akaunti yake ya Instagram unaosomeka “Sina shaka najua mzani ulikoelemea....!!!#uzalendokwanza #Hilinalolititapita.

Muda mchache ulipopita, Babu Tale ambaye ni Meneja wa Diamond, aliposti na yeye picha iliyomuonyesha amebeba mabegi na tiketi ikionekana na kuandika ujumbe ulioashiria kuwa anakwenda kwa Zari, Afrika Kusini kumuombea msamaha Diamond, kwani yeye huwa hashindwi kitu ila aliamua kuwaacha Zari na Diamond wajifunze maisha, halafu ndio aingilie kati kuweka mambo sawa ili warudiane.

Hapo sasa ndipo wajanja wa mjini wakaanza kuumiza kichwa kusaka ukweli wa drama hizo na kubaini kitu.

Mwanaspoti kama kawa likaingia msituni na kugundua kwamba, kuna kipindi cha Realty Show kinataka kuanza pale Wasafi TV hivyo, mpango mzima wa kutengeneza kiki ukaanza kufanya kazi. Kipindi hicho kitahusisha mambo mbalimbali ikiwemo drama zinazoendelea ndani ya familia ya Diamond na WCB nzima.

Hata hivyo, Diamond ambaye kwa sasa yuko jijini London, Uingereza, ameahidi kuwa akitia timu tu atafunguka inshu zote ambazo zimekuwa zikiwatoa watu povu huko kwenye mitandao ya kijamii. Lakini, bado kuna watu wameingia kwenye drama hizo wazima wazima wakikinukisha kinoma huko kwenye mitandao, yaani hakuna kulala unaambiwa.