Instagram yatoa fedha chafu kwa Selena Gomez, Kim Kardashian na Cristiano Ronaldo

Muktasari:
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na HopperHQ's, umeonyesha mwanamuziki Selena Gomez anaongoza kwa kupokea fedha kutoka katika mtandao wake wa Instagram.
New York, Marekani. Unaweza usiamini lakini ndivyo ukweli ulivyo mitandao ya kijamii imekuwa chanzo kingine cha kuingizia watu fedha mbaya zaidi ya dola 550,000.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na HopperHQ's, umeonyesha mwanamuziki Selena Gomez anaongoza kwa kupokea fedha kutoka katika mtandao wake wa Instagram.
1. SELENA GOMEZ
Akiwa na mashabiki123 milioni, ndiye anayeongoza kwa kuwa na watu wengi wanaomfutilia katika mitandao ya kijamii.
Mwanamuziki huyo mwenye miaka 24, anapokea zaidi ya dola 550,000 kwa kila picha anayoituma.
2. KIM KARDASHIAN
Anawatu zaidi ya 100 milioni wanaofuatilia katika mtandao huo naye anapokea dola 500,000 kwa kila picha anayotuma.
3. CRISTIANO RONALDO
Nyota huyo wa Ureno na Real Madrid, anamashabiki wake106 milioni wanaofuatilia ameshika nafasi ya tatu kwa watu wanaovuna fedha kupitia mtandao wa Instagram, akipokea dola 400,000, kwa picha.
4. KYLIE JENNER
Mdogo wake Kim Kardashian anapokea dola 400,000 kwa picha anayotuma inafuatiliwa na watu 95 milioni.
5. KENDALL JENNER anapokea dola 370,000.
6. KHLOE KARDASHIAN anapokea dola 250,000.
7. KOURTNEY KARDASHIAN anapokea dola 250,000.
8. CARA DELEVINGNE apokea dola150,000.
9. GIGI HADID anapokea dola120,000 kwa kila picha katika Instagram.
10. LEBRON JAMES anapokea dola120,000 kwa picha yake moja atakayoituma katika mtandao wa Instagram.