Ibrahimovic ndiye mfalme wa Milan

Muktasari:
Kwa ujumla Zlatan amecheza mechi 10 na kufunga mabao saba katika pambano baina ya timu hizo, huku akiwa kwenye timu ya ushindi mara sita.
MILAN, ITALIA . ZLATAN Ibrahimovic, ndiyo mfalme wa Dabi ya Milan maarufu kwa jina la Derby della Madonnina, hii inatokana na rekodi zake kwenye mechi hiyo kubwa zaidi nchini Italia.
Kwanza Zlatan ndiye mchezaji pekee ambaye amefunga bao kwenye dabi hiyo katika miongo mitatu tofauti. Si mchezo! Lakini pia staa huyu anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji mzee zaidi kufunga bao kwenye mechi ya Serie A baina ya timu hizo.
Kwa ujumla Zlatan amecheza mechi 10 na kufunga mabao saba katika pambano baina ya timu hizo, huku akiwa kwenye timu ya ushindi mara sita.
Akiwa Inter Milan, straika huyo amecheza mechi tano na kufunga mabao mawili, huku akiwa kwenye timu ya ushindi mara 4, wakati akiwa AC Milan amecheza mechi tano pia na kufunga mabao matano huku akiwa kwenye timu ya ushindi mara mbili.