Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huko Simba hadi raha, mbadala wa Mkude apatikana

Huko Simba hadi raha, mbadala wa Mkude apatikana

Muktasari:

VIGOGO wa Simba waliohudhuria mazoezi ya Simba juzi na jana wameanza kutabasamu baada ya kuona mbinu mbadala za Kocha Sven Vandenbroeck kuziba pengo la fundi, Jonas Mkude aliyesimamishwa.

VIGOGO wa Simba waliohudhuria mazoezi ya Simba juzi na jana wameanza kutabasamu baada ya kuona mbinu mbadala za Kocha Sven Vandenbroeck kuziba pengo la fundi, Jonas Mkude aliyesimamishwa.

Katika mazoezi hayo Sven amebadili mifumo na kujaribu mingine tofauti ambayo imeonyesha mwanga.

Kukosekana kwa Mkude kutokana na shutuma za utovu wa nidhamu huenda kusiwaathiri kwenye mechi ya Jumatano dhidi ya FC Platinum ambayo mshindi anafuzu makundi Afrika.

Sven anapenda kutumia mfumo wake pendwa wa (4-2-3-1), ambao una mabeki wanne, viungo wakabaji wawili, viungo washambuliaji watatu na straika mmoja.

Alisema kukosekana kwa Mkude kutatoa nafasi kwa wachezaji wengine kama ambavyo alifanya katika mechi mbili zilizopita na kikosi chake kina wachezaji wengi wazuri ambao wanatumika katika eneo hilo la kiungo.

Anasema katika maingizo ya viungo wengine maana yake watakuwa na plani za mifumo mitatu tofauti ambayo watakuwa wakiitumia katika mechi zilizokuwa mbele yao na hilo walianza kulifanyia kazi tangu katika mechi ya Majimaji na Ihefu ambazo zote walipata ushindi.

“Katika kikosi changu nimebaki na viungo wawili wakabaji Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin ambao nao wote wanaumwa kwa maana hiyo nalazimika kutumia mfumo wa kwanza (3-5-2), ambao utaziba eneo hilo la kiungo mkabaji lakini tutakuwa imara kwenye viungo wa kushambulia na washambuliaji,” alisema.

“Tunaweza kubadili mfumo huo tukacheza mingine miwili (4-3-2) au (4-4-2) na hiyo yote kulingana na wapinzani ambavyo watakuja na watacheza kwa kubadilika na tulifanikiwa kufanya vizuri katika michezo miwili iliyopita ambayo yote tuliingia bila kiungo mkabaji asilia,” alisema Sven.

Mfumo wa kwanza (3-5-2), ambao Sven ameeleza unakuwa na mabeki wa kati asili watatu, viungo watatu huku mabeki wa pembeni Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Shomary Kapombe nao wanaongezeka katika eneo hilo la kiungo (wing backs) huku anakuwa na washambuliaji wawili mmoja akiwa straika asilia kama ni Meddie Kagere, John Bocco au Chriss Mugalu.

Mfumo wa (4-3-2), ambao ulitumika katika kipindi cha pili kwenye mechi na Ihefu wanakuwepo mabeki wanne, kiungo mmoja mkabaji na nafasi hiyo alikuwepo Said Ndemla, viungo wawili washambuliaji, straika asilia mmoja na kiungo mwingine ambaye atakuwa anacheza kutokea pembeni na alimtumia Luis Jose Miquissone.

Mfumo wa mwisho ni (4-4-2), ambao unakuwa na mabeki wanne, viungo wanne na washambuliaji wawili.

Huko Simba hadi raha, mbadala wa Mkude apatikana

Kuhusu mechi ya FC Platinum, Sven alisema; ”Tumefanyia kazi makosa tuliyoonyesha katika mchezo uliopita ambao kwangu naamini tulikuwa na kila sababu ya kushinda.”

WAPEWA MBINU

Wakati FC Platinum wakitua nchini jana, Simba wamepewa mbinu za kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono nyumbani.

Simba inahitaji ushindi wenye utofauti wa kuanzia mabao mawili katika mechi yao ya marudiano ya raundi ya kwanza itakayochezwa Jumatano saa 11.00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini ili iweze kutinga hatua ya makundi ya mashindano hayo baada ya kuchapwa bao 1-0 ugenini Zimbabwe.

Winga wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa ni kocha wa Pamba, Ulimboka Mwakingwe alisema; “Wale Platinum kiwango chao cha ufiti kiko juu sana hivyo benchi la ufundi linatakiwa kuhakikisha wachezaji wanakuwa fiti zaidi ya wale, wasibutue na wacheze mpira wa chini kwa haraka na wawe wepesi.

“Lakini pia mashabiki wanatakiwa wajitokeze kwa wingi kwenda kuipa sapoti timu jambo litakalowaongezea morali ingawa pia wanatakiwa kutumia vyema nafasi ambazo watazitengeneza,” alisema Mwakingwe.

Kiungo wa zamani wa AFC ya Arusha, Ally Ruvu alisema; “Simba bado wana mechi ngumu. Jamaa wale wanacheza vizuri. Waliingia katika mechi ya kwanza wakiwa wanaiheshimu Simba. Lakini kwa sasa Simba kwa maandalizi wanaonekana wako vizuri na morali ya timu iko juu.

“Kwa Simba nina imani nafasi walizotengeneza kule Zimbabwe ugenini kama wakipata hapa watapata matokeo mazuri. Mechi itakuwa nzito kwa sababu wale Platinum wana uzoefu wa haya mashindano. Simba inaingia kwenye huu mchezo ikiwa na faida ya kucheza nyumbani na ukiangalia kuna mechi za ligi. Kocha Sven Vandenbroeck kuna watu hawajawatumia ili awapumzishe

“Simba kwanza wahakikishe Platinum hawachezi vizuri wawabane kwenye eneo lao, wasipate nafasi ya kuingia katika eneo la Simba.

“Viungo wa Simba wawe imara na wawabane Platinum wasiwe wanaingia katika eneo la hatari. na mastraika watumie vyema nafasi zao ambazo watapata lakini pia ningeshauri waanzishe kikosi chenye washambuliaji wawili ili kuwafanya mabeki wa kati wa Platinum wasisogee juu,” alisema Ruvu.

Katika mchezo wa kwanza, Simba ilionekana kuzidiwa kasi na wachezaji wa Platinum pale walipokuwa na mpira hata walipokuwa hawana mpira lakini pia safu ya ushambuliaji ya wawakilishi hao wa Tanzania ilipoteza nafasi kadhaa za mabao ambazo zilitengenezwa na kujikuta ikipata mlima mrefu wa kupanda katika mechi ya marudiano nyumbani.

PLATINUM KINYOONGE

Msafara wa FC Platinum uliwasili jana saa 9.30 ukitokea Zimbabwe ukiwa na kikosi chenye nyota 23 bila Ofisa Habari wao, Chido Chizondo ambaye amegundulika kuwa na corona na wamemwacha kwao karantini.

Msafara huo wa Platinum unaundwa na wachezaji Rahman Kutsanzira, Rainsome Pavari, Petros Mhari, Nomore Chinyerere, Perfect Chikwende, Donald Dzvinyai, Kelvin Madzongwe, Raphael Muduviwa, Tawana Chikore, Future Sibanda, Denzel Khumaro na William Stima.

Wengine ni Gift Bello, Francis Tizayi, Elie Ilunga, Gift Mbweti, Elias Maguli, Silas Songani, Evidence Tendayi, Kelvin Mangiza, Lawrence Mhanga, Ralph Kawondera na Panashe Mutimbanyoka.