Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huko mtandaoni unapata hadi safari za bure

Pambana Pict
Pambana Pict

Muktasari:

  • Akizungumza kuhusu fursa hiyo, Meneja Uendeshaji wa Biashara Piku Afrika, Sia Melewas amesema koponi hiyo ni maalum kwa wafanyabiashara na wananchi wa kawaida kabisa wanaotaka kurahisisha shughuli zao za kila siku kwa kupitia usafiri wa Bolt.

Moja ya majukwaa la kidijitali yanayoendesha minada ya kipekee mitandaoni limezindua bidhaa yake mpya itakayowapa washiriki nafasi ya kujishindia koponi yenye thamani ya Sh100,000 kwa matumizi ya kila siku ya kunufaika na usafiri.

Akizungumza kuhusu fursa hiyo, Meneja Uendeshaji wa Biashara Piku Afrika, Sia Melewas amesema koponi hiyo ni maalum kwa wafanyabiashara na wananchi wa kawaida kabisa wanaotaka kurahisisha shughuli zao za kila siku kwa kupitia usafiri wa Bolt.

Amesema kupitia combo hilo la mtu anaweza kujipatia safari zenye thamani ya Sh100,000, hivyo amewataka watu kuchangamkia fursa hiyo ya kipekee yenye lengo la kuendelea kuwarahisishia wateja wao huduma.

“Vijana, wanawake kwa wanaume tunawakaribisha kuanza sasa kuingia katika mnada wetu huu ili kuweza kujipatia koponi hiyo na bidhaa zingine zingi, washiriki wote kuanzia umri wa miaka 18 wanakaribishwa kushiriki kwa kupakua App ya Piku kupitia Play Store (kwa watumiaji wa Android) au App Store (kwa watumiaji wa iPhone).

“Tiketi za ushiriki zinapatikana kwa bei nafuu; Sh1,000 kwa tiketi 10, Sh5,000 kwa tiketi 50, na Sh100,000 kwa tiketi 100. Kadri unavyoongeza tiketi, ndivyo nafasi ya kushinda inavyoongezeka,” amesema Melewas

Hata hivyo, Melewas amesema jukwaa hilo limepanga kumaliza mwaka 2025 kwa kishindo na mshindi mmoja atajinyakulia gari aina ya Toyota Raum, lenye bima ya mwaka mzima na kadi ya mafuta, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh30 milioni.

Aidha, mwanzoni mwa Desemba mwaka huu, “Mgodi wa Piku” utatoa zawadi ya seti ya dhahabu safi yenye thamani ya Sh6 milioni na mshindi atapata uhuru wa kuchagua seti anayoitaka dukani.

Vilevile, kila baada ya siku tatu, mshiriki anaweza kujishindia simu janja aina ya Samsung A06 yenye thamani ya Sh250,000, huku baada ya siku 28, kupitia “Zigo la Piku”, mshindi atakayetoa dau dogo na la kipekee ataondoka na pikipiki mpya aina ya TVS yenye helmet, reflector, bima, na kadi ya mafuta ya miezi sita, vyote vikiwa na thamani ya Sh4 milioni.

Kwa upande mwingine, Melewas amesema kila baada ya siku 14 katika kombo la mnada huo, washiriki wana nafasi ya kushinda saa ya kisasa, manukato ya kifahari, televisheni ya LG inchi 55 na Airtel Router iliyolipiwa mwaka mzima, zenye jumla ya thamani ya Sh2.4 milioni.
Mwishooo…