Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi rekodi kina Pogba watasota kuzivunja

LONDON, ENGLAND
MECHI za wiki namba nne kwenye Ligi Kuu England zinapigwa wikiendi hii. Liverpool walifanya walichokifanya nyumbani kwa Leicester City jana Jumamosi huku Manchester City nao walikuwa na shughuli na Newcastle United.
Ni mechi baada ya mechi, ambapo leo Jumapili kutakuwa na vigogo wengine wakiingia uwanjani ambapo Arsenal na Manchester United watacheza na Cardiff City na Burnley kwa kufuata mtiririko. Lakini, ligi hiyo zitachezwa na kuhusisha mastaa kibao, ambao watapambana na hali zao kujaribu kufikia rekodi hizi ngumu kabisa za wakali waliocheza mechi nyingi katika historia ya ligi hiyo. Ni rekodi ambazo wakali kama Paul Pogba watasota kuzivunja kutokana na majina yao kuhusishwa na mpango wa kuachana na ligi hiyo na kutimkia kwingineko kama Italia, Hispania na Ufaransa.

5.Gary Speed- mechi 535
Gary Speed ameshafariki dunia. Lakini, jina lake bado lipo kwenye chati za juu kwenye historia ya Ligi Kuu England akiwa mchezaji namba tano aliyecheza mechi nyingi kwenye ligi hiyo. Speed alicheza mechi 535 za ligi hiyo akipita katika vikosi vya Leeds United, Everton, Newcastle United, Bolton Wanderers na Sheffield United. Alishinda taji ya Ngao ya Hisani mwaka 1992, Ligi Daraja la Kwanza 1992 na Ligi  Daraja la Pili mwaka 1990. Alifariki dunia mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 42.

4.David James- mechi 572
Kipa wa zamani wa kimataifa wa England, David James ni mmoja kati ya mastaa waliocheza mechi nyingi sana kwenye historia ya Ligi Kuu England. Kipa huyo alianzia maisha yake ya soka huko Watford kisha akaenda kujiunga na Liverpool mahali ambako alipata mafanikio makubwa. Aliichezea pia Portsmouth, Manchester City na West Ham United. Kwenye Ligi Kuu England amecheza mechi 572, aliwahi kushinda ubingwa wa Kombe la Ligi akiwa na Liverpool mwaka 1995 na Kombe la FA akiwa na Portsmouth mwaka 2008.

3.Frank Lampard- mechi 609
Gwiji wa Chelsea, Frank Lampard anashika namba tatu katika orodha ya mastaa waliocheza mechi nyingi sana kwenye Ligi Kuu England. Kiungo Lampard ameitumikia West Ham United, Swansea, Chelsea na Manchester City. Amebeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja, Europa League mara moja na Ligi Kuu England mara tatu, huku Kombe la FA akibeba ubingwa mara nne, Kombe la Ligi mara mbili na Ngao ya Jamii mara mbili. Lakini, kubwa ni idadi ya mechi 609 alizocheza kwenye Ligi Kuu England kabla ya kung'atuka kwenye ligi hiyo. Kwa sasa ni kocha wa Derby County.

2.Ryan Giggs- mechi 632
Gwiji wa Manchester United, Ryan Giggs amechezea klabu moja tu kwa maisha yake yote ya soka. Aliibukia kutoka kwenye timu ya watoto ya Man United na kuwa staa wa kutumainiwa katika kikosi cha wakubwa cha wababe hao. Alistaafu soka mwaka 2014, lakini ni baada ya kuweka rekodi kwa kucheza mechi 632 kwenye Ligi Kuu England. Katika maisha yake ya soka, Giggs amebeba mataji 13 ya Ligi Kuu, manne ya Kombe la FA, matatu ya Kombe la Ligi, Ngao ya Jamii mara tisa na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, UEFA Super Cup moja, Klabu Bingwa Dunia mara moja.

1.Gareth Barry- mechi 653
Gareth Barry ndiye mchezaji pekee kwenye orodha hii ambaye bado anacheza hadi sasa. Amecheza mechi 653 hadi sasa. Alianzia soka lake huko Aston Villa kisha alihamia Manchester City alikobeba ubingwa wa Ligi Kuu England mwaka 2012 na Kombe la FA mwaka 2011. Kiungo alikwenda kujiunga na Everton pia na kuitumikia kwa miaka minne kabla ya kusaini kuitumikia West Brom. Amevunja rekodi ya Ryan Giggs ya kucheza mechi nyingi kwenye historia ya Ligi Kuu England.