Hivi hapa vikosi vya KMC, Ihefu

DAKIKA chache zimesalia kuanza kwa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu bara kati ya KMC na Ihefu ambapo makocha wa timu zote mbili tayari wameweka wazi vikosi vitakavyoanza.
KMC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya tano na pointi 45 kwenye msimamo wa Ligi hivyo inahitaji ushindi ili kujihakikishia kumaliza katika nafasi hiyo huku Ihefu ikiingia ikiwa nafasi ya 16 na alama 35.
Ihefu inahitaji ushindi kwenye mchezo huu ili kukwepa kushuka daraja moja kwa moja na kupata alama tatu zitakazoipeleka kucheza mechi za mtoano wakati huo ikiziombea kupoteza timu tatu zilizo juu yake.
Jeshi la Ihefu ambalo litaingia uwanjani leo kutafuta alama tatu muhimu chini ya kocha Zuberi Katwila ni Deogratius Munishi, Mando Mkumbwa, Omary Kindamba, Samweli Onditi, Oscar Masai.
Wengine ni Raphael Daud, Joseph Mahundi, Omary Hassan, Andrew Simchimba, Juma Mahadhi na Tepsi Evance.
Watakaoanzia nje ni Isihaka Luhamba, Emanuel Charles, Wema Sadoki, Willy Mgaya, Enock Jiah, Issa Ngoa na Shaban Hamis.
Kwa upande wa wenyeji KMC kocha John Simkoko amewaanzisha Sudi Dondola, Kelvin Kijiri, Ally Ramadhan, Lusajo Mwaikenda, Ismail Gambo, Hassan Kapalata.
Wengine ni Kenny Ally, Martin Kigi, Charles Ilamfya, Abdul Hilaly na Sadala Lipangile huku Israel Mwenda, Hassan Kabunda, Mohamed Samatta, Jean Mugiraneza na Clif Buyoya wakianzia benchi.