Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Heh! Coutinho anafanana na Oscar?

Coutinho

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Ephraim Makoye amestuka  baada ya kumwona kiungo mshambuliaji  mpya wa Yanga  Mbrazil, Andrey Coutinho, akadhani wamemsajili Oscar wa Chelsea.

Makoye amewaambia Simba: “Sasa mmekwisha.”

“Ukimwangalia amefanana kabisa na Oscar kuanzia sura hadi mwili wake ila sijamwona kama anaweza kuwa na kiwango kama cha Oscar ngoja tumwone uwanjani anaonekana ni mchezaji mzuri  na mimi namjua kocha maximo hawezi kuleta mtu wa ovyo,”alisema Makoye.

Makoye amesema ameanza kuona mwanga wa mafanikio baada ya kutua kwa kocha Marcio Maximo lakini akaonya asihukumiwe kwa mechi mbili au tatu badala yake apewe nafasi ya miaka miwili ili kuleta mafanikio zaidi.

“Tumwache kwanza Maximo tumpe nafasi ili alete neema kwenye timu yetu ya Yanga amekuja kocha ninayemwamini sana sasa tutatisha pale Jangwani tumpe muda wa kutengeneza kikosi chake hatari ambacho kitakuwa ni tishio kubwa haswa kwa Simba,”alisema Makoye.