Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hata kama uhondo wa Afcon ulikuwa hapa

Muktasari:

  • Makala haya inakuleta baadhi ya mambo ambayo yalitokea kwa siku 14, ambazo fainali hizo za Afcon U-17, zilifanyika na kutoa timu nne zinazokwenda kuiwakilisha Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia 2019 nchini Brazil Oktoba mwaka huu.

DAR ES SALAAM. FAINALI za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri chini ya miaka 17 (Afcon U-17) yamefanyika kwa mara ya kwanza nchini na kushuhudiwa kikosi cha Cameroon kikitwaa ubingwa huo kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza 2003 michuano ilipofanyika nchini eSwatini (zamani Swaziland).

Michuano hii ilianza Aprili 14, kwa wenyeji timu ya vijana ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ kucheza dhidi ya Nigeria, baada ya ufunguzi wa aina yake uliohusisha burudani mbalimbali kutoka kwa vikundi vya ngoma, Halaiki na msanii wa kizazi kipya wa kundi la WCB, Rayvanny, ambaye alitumbuiza.

Uwepo wa mashindano hayo nchini ulileta ugeni mkubwa wakiwamo maofisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wakiongozwa na Rais Ahmad Ahmad na wageni wengine mbalimbali ambao walipata nafasi ya kwenda kutembelea vivutio vya utalii nchini, lakini hata biashara zilifanyika kama hoteli walizofikia timu na wageni, vyakula, manunuzi mbalimbali na mambo mengine mengi nje ya uwanja.

Makala haya inakuleta baadhi ya mambo ambayo yalitokea kwa siku 14, ambazo fainali hizo za Afcon U-17, zilifanyika na kutoa timu nne zinazokwenda kuiwakilisha Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia 2019 nchini Brazil Oktoba mwaka huu.

KUTOLEWA SERENGETI

Kabla ya kuanza kwa mashindano haya kulikuwa na hamasa kubwa kwa mashabiki wa soka kutoka Tanzania wakiamini kikosi cha Serengeti kitakwenda kufanya vizuri, kutwaa ubingwa au kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia.

Katika mechi ya ufunguzi Serengeti Boys ilikubali kufungwa mabao 5-4 dhidi ya Nigeria huku mashabiki wakionekana kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishaingilia timu hiyo yenye nyota kama Kelvin John ‘Mbappe’, Morice Abraham, Edmund John na wengine wengi.

Licha ya kutanguliwa 1-3 dhidi ya Nigeria wakati wa mapumziko, vijana wa Serengeti hawakutaka tamaa. Walikomboa magoli yote mwanzoni mwa kipindi cha pili na kuongoza kwa 4-3.

Hata hivyo, benchi la ufundi lilionekana kuwaacha vijana waendelee kufunguka na kushambulia wakitaka magoli zaidi badala ya kucheza kwa nidhamu ya kulinda walichonacho.

Matokeo yake, mashambulizi ya kaunta yakawadhuru. Nigeria wakafunga magoli mawili ya haraka haraka na kukamilisha ushindi wa 4-5.

Vijana walionekana kufadhaishwa na matokeo hayo na wakapoteza ushujaa ule walioonyesha dhidi ya Nigeria wa kuzinduka kutoka kufungwa magoli na kuongoza 4-3.

Wakikosa hamasa ya mechi yao ya kwanza, Serengeti Boys wakapoteza mechi zote mbili zilizofuata dhidi ya Uganda na Angola, wakirudia makosa yale yale waliyokuwa wakiyafanya katika mechi ya kwanza.

Serengeti ilifungwa mabao 12 na yenyewe kufunga magoli sita.

Ilitarajiwa presha kwa kocha Oscar Mirambo baada ya fainali hizo, akishinikizwa na baadhi ya wadau ajiuzulu.

Kimsingi kuondolewa kwa Serengeti Boys katika hatua ya mwanzo na kushindwa kufanya hata kufikia malengo yale mawili ya kutwaa ubingwa au japo kutinga nusu fainali na hivyo kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2019, kuliondoa mzuka na morali ya mashindano haya kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kuanza.

Timu mbili kutoka ukanda wa CECAFA, wenyeji Serengeti Boys na Uganda zote ziliishia katika hatua ya makundi na kushuhudia timu tatu za Cameroon, Guinea na Nigeria kutoka Afrika Magharibi na Angola zikitinga hatua ya nusu fainali.

MASHABIKI WAYEYUKA

Baada ya kikosi cha Serengeti Boys kushindwa kufanya vizuri na kuondolewa katika hatua ya awali, mashabiki wa soka ambao awali walionekana kuwa na hamu ya kwenda kwenye Uwanja wa Taifa na Azam Complex hawakuonekana tena.

Siku ya ufunguzi wa Afcon kulikuwa na viingilio lakini mara baada ya siku hiyo kupita Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, alitangaza hakutakuwa na viingilio tena katika mashindano hayo lakini mashabiki hawakuwa wanakwenda kwa wingi kushuhudia mechi hizo.

NUSU FAINALI

Mara baada ya kumalizika mechi za hatua ya makundi kwa timu nne za Nigeria, Angola, Cameroon na Guinea zilizopita katika hatua ya nusu fainali zilikwenda kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi zote mbili kumalizika kwa suluhu na kupatikana timu mbili zilizokwenda kucheza fainali na mbili zilizocheza mechi ya mshindi wa tatu.

Nusu fainali ya kwanza ilikuwa kati ya Nigeria dhidi ya Guinea ambayo dakika tisini ilimalizika kwa suluhu na kwenye hatua ya ‘matuta’ Guinea walishinda kwa kufunga penalti zote 10-9, huku katika nusu fainali ya pili mabingwa Cameroon walishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Angola.

CAMEROON BINGWA

Kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon kilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B, wakiwa na pointi saba wakicheza mechi tatu ambazo mbili walishinda na kutoka sare mmoja huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote, walifunga mabao manne na wao kufungwa moja.

Mechi ya kwanza Cameroon ilianza vizuri kwa kumfunga Guinea mabao 2-0, mechi ya pili ilishinda tena 2-1, dhidi ya Morocco na mchezo wa mwisho ikatoka suluhu dhidi ya Senegal. Katika hatua ya nusu waliwang’oa Angola kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 za mechi yao kumalizika kwa suluhu. Kanuni za mashindano hayo ya vijana hakuna dakika 30 za nyongeza baada ya 90.

Mechi ya fainali iliwakutanisha Cameroon dhidi ya Guinea ambao walikutana nao katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano hayo. Dakika tisini zilimaliza bila kufungana na katika hatua ya mikwaju ya penalti Cameroon walishinda 5-3, na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

MSIKIE LIUNDA

Mratibu wa Mashindano ya Afcon u-17, Leslie Liunda, alisema Serengeti Boys ilifanya maandalizi ya kutosha lakini ilikuwa bahati mbaya kukutana na kila timu ambayo ilikuwa na kiu ya kufika fainali na kuchukua ubingwa wa mashindano hayo ndiyo maana wakashindwa kufanya vyema kama ilivyotegemewa.

“Kufanikiwa kama nchi tumepiga hatua na kupata fursa nyingi kupitia mashindao haya katika maeneo mbalimbali na limekuwa jambo muhimu kwetu na kufungua milango mingi mbali ya timu yetu Serengeti kushindwa kufikia malengo ambayo kila Mtanzania alitamani kuona,” alisema.

“Upande wetu kama waandaaji tumefanikiwa kwa asilimia 99, kwani maofisa wa Shirikiso la Soka Afrika (CAF), pamoja na Rais Ahmad wamerizika kwa kiwango cha juu kwa yale yote ambayo tuliyafanya muda wote wa mashindano tena kwa mara ya kwanza,” anasema Liunda.