Haji Manara auteka Uwanja wa Taifa kwa shangwe

Muktasari:
Kitendo cha Manara kuingia uwanjani mashabiki waliamka na kuanza kumshangilia kama vile rais anaingia kwa kumpugia vitambaa na mikono.
Dar es Salaam.Afisa habai wa Simba, Haji Manara ameamsha shangwe la aina yake baada ya kuingia akiwa na walinzi wawili ambao wamevalia suti nyeusi na miwani wakati akiingia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kitendo cha Manara kuingia uwanjani mashabiki waliamka na kuanza kumshangilia kama vile rais anaingia kwa kumpugia vitambaa na mikono.
Manara baada ya kuzunguka uwanja mzima kwa kupunga mikono alianza kucheza kama kawaida yake, jambo liliendelea kuwapagawisha mashabiki wake.
Manara amefunika kwa nyota yake kukubalika mbele ya mashabiki wa Simba ambao walionekana kama walikuwa na hamu ya kumuona Afisa habari huyo.
Mara aliongeza shangwe kwa mashabiki tofauti na alivyokuwa mwanzo ambapo kelele za shangwe hasikusikika kama alivyokuwa ameingia yeye
Katika tamasha hilo mbali ya kupigwa kwa nyimbo za Simba na wasanii mbalimbali kama Juma Nature, Diamond ziliteka tamasha hilo.
Ukiachana na burudani ya muziki ambao mashabiki wanaendelea kuipata bado watu wanaendelea kuingia uwanjani hapo.
Simba inahitimisha siku yao ya Simba Day inayofanywa kila mwaka ambapo wanaitumia kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kutambulisha wachezaji.