Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Giniki atwaa dhahabu Poland, avunja rekodi

Mwanariadha nyota wa Tanzania, Emmanuel Giniki Gisamoda ametwaa medali ya dhahabu na kuvunja rekodi nchini Poland.

Giniki ametawazwa kuwa bingwa mpya wa mbio ya nusu marathoni ya Warsaw zilizofanyika leo.

Mbio hizo za kimataifa zimeshirikisha zaidi ya wanariadha 10,000 kutoka nchi zote duniani.

 Mbali na ushindi, Giniki pia amevunja rekodi ya mbio hiyo iliyodumu kwa miaka minane.

Giniki alifanikiwa kukata utepe na kumaliza kilomita 21, akitumia saa 1:00:30 muda  iliomuwezesha kuvunja rekodi iliyowepo yenye saa 1:00:49.

Nafasi ya pili katika mbio hizo ilichukuliwa na Chibete Abel kutoka Uganda aliyemaliza  sekunde 10 nyuma ya Giniki akitumia saa 1:00:40 huku nafasi ya Tatu ikichukuliwa na Too Josphat Kipchirchir kutoka Kenya aliyemaliza kwa saa 1:01:46.