Gidabuday aibukia kwenye uchaguzi TFF

Friday June 11 2021
UCHGAGUZI PIC
By Oliver Albert
By Imani Makongoro

Katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelim Gidabuday ameibukia kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Gidabuday amejitokeza kwenye mchakato wa kuchukua fomu unaoendelea makao makuu ya TFF, Dar es Salaam.

"Niko hapa kumsapoti rafiki yangu ambaye ametangaza nia kutaka ujumbe," alisema Gidabuday.

Mgombea huyo ni Ally Hoza aliyewahi kugombea ubunge wa jumbo la Korogwe vijijini kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 na 2020 Kibamba lakini kura hazikutosha.

Mgombea mwingine aliyetinga TFF kuchukua fomu ni mwanachama wa Yanga, Jummy Kindoki ambaye ametangaza nia kwenye ujumbe.

Advertisement