Sita waitaka nafasi ya Karia TFF

Thursday June 10 2021
tff pic
By Imani Makongoro

Mambo yanazidi kunoga kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Agosti 7 mjini Tanga ambapo vigoGo sita wameonyesha nia ya kuutaka urais wa Shirikisho hilo kuchuana na rais anayetetea kiti chake, Wallace Karia.

Hadi leo saa 10 jioni TFF imetoa orodha ya watu ambao wamechukua fomu wakiwemo wawili waliochukua leo Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba na mchambuzi wa soka, Ally Mayay.

Wengine ni  mchambuzi wa soka, Oscar Oscar, Deogratius Mutungi, Evans G Mgeusa na Zahoro Mohammed Haji.

Kwenye nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji hadi leo jioni waliokuwa wamejitokeza ni watano akiwamo Lameck Nyambaya ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Athuman Kambi, Liston Katabazi, Michael Petro, Sandy Kimji wote ni kwa kanda namba moja inayojumuisha Lindi, Dar es Salaam, Morogoro, Mtwara na Pwani.

Kanda namba mbili (Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga) aliyechukua fomu ni Khalid Abdallah Mohammed, kanda namba nne (Dodoma, Shinyanga, Simiyu, Singida) waliochukua ni Mohamed Aden na Osuri Kosuri na kanda namba tano ina mikoa ya Geita, Kagera, Mara na Mwanza ambapo aliyechukua ni Salum Chama
 


Advertisement
Advertisement