Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita Gold mabingwa FDL

Muktasari:

  • Timu zote zilishapanda Ligi Kuu lakini alikuwa anatafutwa bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza.

TIMU ya Geita Gold imetwaa ubingwa wa Ligi Daraja la kwanza (FDL) baada ya kuifunga Mbeya Kwanza 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Uhuru leo Mei 30, 2021.


Katika dakika 90 za mchezo huo hakukuwa na timu iliyoona lango la mwenzake hadi dakika 111 mshambuliaji wa Geita, Omary Ramadhan alipowanyanyua mashabiki wa timu hiyo akionganisha kwa kichwa krosi ya Jeremiah Mussa na mpira ukaenda waving moja kwa moja.


Kikanuni mchezo ulipomalizika katika dakika 90 uliendelea kwa dakika 30 ili apatikane bingwa katika mtanange huo ambao ulikuwa na ufundi pamoja na ubabe kidogo.


Timu hizo katika kipindi cha kwanza zilitoka sare ya bila kufunga licha ya kuwa na mashambulizi ya hapa na pale wakitafuta bao.


Katika kipindi cha pili dakika 60 Geita walifanya mabadiliko ya kumtoa Said Mussa na kuingia Suluja Muhoja katika eneo la kiungo.


kwenye kipindi hichi Geita walionekana kumiliki mpira lakini kwenye upande wa umaliziaji ilionekana kuwa na changamoto mbele ya mabeki wa Mbeya Kwanza.


Pengo la mshambuliaji Atupele Green kwenye kikosi cha Geita Gold lilionekana kutokana na washambuliaji wallop kutokuwa na makini wanapofika ndani ya boksi.


Atupele licha ya kusajiliwa dirisha dogo na kucheza mechi nane ameifungia timu hiyo magoli matatu na kutoa pasi tatu za mabao.


Dakika 74 Chilo Mkama wa Geita alipiga shuti kali nje ya boksi lakini shuti hilo nilipitia pembeni kidogo na lango la Mbeya Kwanza.


Dakika 76 Geita ilifanya mabadiliko alitoka Shaban Maulid na kuingia Frank Aloyce wakati huo huo Mbeya Kwanza akitoka Oscar Mwajanga na kuingia Sudi Mlindwa, mabadiliko yote takiwa katika eneo la ushambuliaji.


Dakika 84 mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Pita Mwaikana alitaka kufunga bao la kuongoza baada ya kuonganisha kwa kichwa krosi aliyopigiwa na William Edgar.


Mbeya kwanza katika dakika za mwisho waliamua kutumia mipira ya krosi kwenda langoni kwa Geita lakini


Dakika 88 Geita walifanya mabadiliko ya kumtoa Erick Mlilo na kuingia Joseph Majagi ili kuimalisha mchezo huo.


Kiungo wa Mbeya Kwanza, Chesco Mwasimba alitolewa kadi nyekundu baada ya kuonyeshewa kadi ya pili alipomfanyia madhambi Jonathan Dominic.


Dakika 94 mshambuliaji wa Geita, Sulula Muhoja alifyatuka shuti kali nje ya boksi  akipokea pasi ya Frank Aloyce lakini mpira huo uliishia mikononi kwa kipa Hamad Kadedi.


Dakika 98 Mbeya kwanza walijibu mapigo baada ya kufanya shambulizi la kushtukiza kupitia kwa William Edgar ambaye alitoka kwa spidi na kuingia ndani ya boksi kisha alifyatuka shuti kali lililompita tobo kipa wa Geita, Philemon Ramadhan lakini kipa huyo alifurahi mpira na kupaka.


Mbeya kwanza walifanya mabadiliko mengine dakika 103 kwa kumtoa Fredrick Magata na kuingia Felix Felix, wachezaji wote walikuwa wanaonekana wamechukua katika dakika hizo.


Dakika 111  mshambuliaji Omary Ramadha 'Berbatov' aliifungia bao la ushindi Geita kwa kichwa akitumia vizuri krosi ya Jeremiah Thomas.

Baada ya mechi hiyo wachezaji walikabidhiwa tuzo ambapo William Edgar wa Mbeya Kwanza alikuwa mfungaji bora kwa mabao 13,  Geofrey Julius wa Geita Gold mchezaji bora huku Fred Minziro akiwa kocha bora.