Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geay amaliza wa saba mashindano ya dunia

Dakika 1:56 zimemkosesha Mtanzania Gabriel Geay kutwaa dhahabu mbele ya bingwa mpya raia wa Ethiopia, Tamirat Tola kwenye mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea nchini Marekani.

Geay aliyetumia saa 2:07:32 kumaliza mbio ya marathoni amekamata nafasi ya saba nyuma ya Tola aliyetumia saa 2:05:36.

Licha ya kukosa medali, Geay ataondoka na dola 6000 ambayo ni zaidi ya Sh 13.8 Milioni mbazo Shirikisho la riadha la dunia hutoa kama zawadi kwa kila mwanariadha atakayemaliza wa saba kwenye kila mbio kwenye mashindano hayo.

Tola mbali na kutwaa dhahabu ameondoka na kitita cha dola 70,000 ambayo ni zaidi ya Sh 161 Milioni, huku Muethiopia mwenzake, Mosinet Geremew akimaliza wa pili akitumia saa 2:06:45.