Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi aisoma Pamba Jiji

Muktasari:

  • Kutokana na hilo, Gamondi amesema wana kila sababu ya kutumia mbinu ya kulazimisha kuwashambulia kuhakikisha hakuna kinachoshindikana katika kusaka ushindi ili kuwa na mwendelezo mzuri kama walivyoanza.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema kutokana na utafiti alioufanya amebaini kwamba wapinzani wanaocheza nao kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Pamba Jiji ni timu ambayo inajilinda zaidi kuliko kushambulia.

Kutokana na hilo, Gamondi amesema wana kila sababu ya kutumia mbinu ya kulazimisha kuwashambulia kuhakikisha hakuna kinachoshindikana katika kusaka ushindi ili kuwa na mwendelezo mzuri kama walivyoanza.

Gamondi ametoa kauli hiyo wakati kesho Alhamisi Yanga ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Pamba Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 12:30 jioni.

Yanga katika mechi tatu za ligi ilizocheza msimu huu, imefunga mabao manne jambo ambalo limeonekana kutowafurahisha mashabiki wa timu hiyo ambao wamezoea kuiona timu yao ikishusha dozi za maana kama ilivyofanya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu hatua za mwanzoni kabla ya kufuzu makundi kwani iliifunga Vital'O jumla ya mabao 10-0 katika mechi mbili na CBE SA jumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili.

"Tunafahamu Pamba Jiji hawajashinda mchezo wowote. Hata hivyo nafahamu uimara walionao kwani hawajaruhusu mabao mengi, katika mechi sita wameruhusu matano pekee lakini wamefunga mawili. Tumefanya utafiti wetu tumegundua ni timu inayokaa sana nyuma, hivyo lazima tulazimishe ushindi," amesema Gamondi na kuongeza;

"Hakuna kitu bora zaidi ya kufunga bao kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Kuna muda unaweza kufunga moja au usifunge kabisa. Kitu ambacho siwezi kuahidi, ni idadi ya mabao, ninachoweza kuwaambia mashabiki ni kwamba tuna uhakika wa kujitoa na kucheza vizuri na kushinda. Hii ni ligi, tuna mechi 30, tumeshacheza mechi 3 tuna alama 9 na tuna furaha.

"Ndani ya muda mfupi tumecheza mechi nne mfululizo, sio ratiba rafiki sana ya wachezaji kujiandaa na kuwa na utimamu kamili wa kimwili. Lakini tupo tayari kwa mchezo wa kesho. Hata hivyo tunajua tutakumbana na mchezo mgumu. Kimsingi haitupi shida sana kwani tumejipanga kiakili na kimwili tupo imara."