Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gama Gaming kusimamia Afya za Kinamama

MENEJA wa Tehama wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Kabora Mboya ameyataka makampuni ya kubahatisha nchini kuhakikisha wanawalinda wachezaji wa mchezo huo ili waweze kupata haki zao na kuiongezea mapato Serikali.

Mboya alifunguka hayo kwenye uzinduzi wa kampuni ya kubahatisha ya Gama Gaming iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa uzoefu mzuri wa michezo ya kubahatisha ili kukidhi haja ya Watanzania kwa michezo hiyo.

Anasema wao kama GBT wamekuwa wakisimamia haki za wachezaji ili kuhakikisha Serikali inanufaika na mchezo huo kwa kukusanya kodi alitumia nafasi hiyo kumtaka mkurugenzi wa kampuni hiyo kuhakikisha anafanya matangazo ya kutosha ili watanzania waweze kupata uelewa namna ya kucheza.

"Kwa niaba ya Serikali tunataka elimu hiyo iwafikie wengi ili ukusanyaji wa mapato uongezeke kupitia kampuni za kubahatisha huku haki za wachezaji ziweze kufuatwa kwa kuhakikisha washindi wanapewa kile wanachostahili kulingana na ushindi," anasema.

Mkurugenzi wa Gama Gaming, Wilfred Magotti anasema mchezo wao wa kubahatisha utakuwa katika droo tatu katika saizi na viwango tofauti kulingana na mchezaji ambapo ni dhahabu ambayo itatumia kiwango cha elfu moja, Almasi elfu mbili na Tanzanite elfu tano kwa kila mchezo.

Anasema kila tiketi ya mchezaji ina nafasi kadhaa ya kushinda mwanzoni na kila tiketi ina nafasi mbili wakati wa jackpot ya papo hapo na kila wiki na nyingine zitaongezwa kulingana na mchezo huo utakavyokuwa unachezwa.

Pia anasema asilimia 10 ya faida watakayoipata kupitia michezo hiyo watatumia kutoa misaada shuleni, Hospitali na kuwekeza katika kusimamia afya za kinamama.

"Kama sehemu ya wajibu wetu wa kijamii tumejipanga kuwa mwanachama hai katika jamii yetu na ndio maana tumejipanga kushiriki katika nguzo hizo tatu ambazo ni elimu, maendeleo ya jamii na huduma ya afya." anasema.