Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fundi wa danadana Hadhara afariki, azikwa usiku huu

ZAHRA Pict

Muktasari:

  • Hadhara aliyejizolea umaarufu mkubwa enzi za uhai wake kwa kipaji cha kuuchezea mpira atakavyo, amekutwa amefariki dunia ndani akiwa peke yake.

FUNDI wa danadana, mwanadada Hadhara Charles ambaye mwili wake umekutwa umefia chumbani tangu siku tatu zilizopita unazikwa usiku huu nyumbani kwake Chanika jijini Dar es Salaam.

Hadhara aliyejizolea umaarufu mkubwa enzi za uhai wake kwa kipaji cha kuuchezea mpira atakavyo, amekutwa amefariki dunia ndani akiwa peke yake.

Mdogo wa Hadhara aliyejitambulisha kwa jina la Mama Raiyan ameliambia Mwanaspoti namna kifo cha dada yake kilivyotokea na kwa jinsi mwili ulivyoharibika mazishi yake yatafanyika kwa haraka.

"Hadhara alikuwa na changamoto ya kifafa ambacho kadri muda unavyokwenda ndivyo kilikuwa kinazidi, Chanika alikojenga alikuwa anaishi peke yake na majirani wamesikia harafu ndipo wakajua amefariki," amesema mdogo wake huyo na kuongeza;

"Kwa namna alivyoharibika anazikwa leo leo hapo hapo nyumbani kwake,  kama ni kifo kitakuwa kimemtokea Jumapili, maana sikukuu ya juzi tumekula naye nyumbani.

"Ndugu waliyopo maeneo jirani kama Mbagala hao ndiyo watabahatika kuzika, mimi mwenyewe nipo Tegeta nina watoto wawili wadogo nimeshindwa kuwahi kwa jinsi inavyoelezwa mwili umeharibika vibaya, baada ya kumpumzisha ndipo tutajua kipi kitaendelea."

Mwanaspoti limewahi kumfanyia mahojiano Hadhara lilishuhudia namna alivyokuwa anahangaika na ugonjwa huo, ambao ulimpata katikati ya mahojiano.

Aliwahi kusema: "Ninasumbuliwa sana na ugonjwa wa kifafa, kuna wakati nilikuwa nikisafiri kwenda nje kwenye shoo changamoto hiyo ilikuwa inanikumba, msaada wangu ilikuwa ni wale ambao naongozana nao."