Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fri-kiki za Morrison balaa

Muktasari:

UNALIKUMBUKA lile bao la frii-kiki ambalo kipa, Aishi Manula alitunguliwa na winga Benard Morisson wakati huo akicheza katika kikosi cha Yanga kwenye mechi ya dabi duru la pili msimu iliyopigwa Machi 8, 2020?

UNALIKUMBUKA lile bao la frii-kiki ambalo kipa, Aishi Manula alitunguliwa na winga Benard Morisson wakati huo akicheza katika kikosi cha Yanga kwenye mechi ya dabi duru la pili msimu iliyopigwa Machi 8, 2020?

Kwenye mazoezi ya wiki hii amefanya mazoezi ya staili hiyo mara kibao na hata kwenye mechi ya leo frii-kiki zote zake.

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mo Simba Arena, Morrison, Clatous Chama, Luis Miquissone, Rally Bwalya na Erasto nyoni walipewa programu maalumu ya kupiga frii-kiki licha ya wote kufanya vizuri lakini Morrisson alipiga frii-kiki kali ya kideoni ambayo moja kwa moja ilikwenda kukwama katika neti.

Bao hilo la frii-kiki ambalo alimtungua kipa kutoka timu ya vijana lilipigwa kiufundi na kufanya mashabiki wa Simba kumshangilia na wengine kumpigia makofi.

Katika programu hiyo, kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane alipanga vifaa malumu kama ukuta nje kidogo ya boksi la 18, kisha kuwahesabia hatua kadhaa wachezaji hao na kutenga mpira ambayo walipiga kwa kupokezana huku golini.

Morrison alipiga frii-kiki kama tano na kufunga tatu na kati ya hizo ni ile moja ya mwisho aliyoipiga kiufundi na kuzama moja kwa moja nyavuni jambo ambalo lilimfanya kupandwa na mzuka.

Mzuka huo wa Morrison aliokuwa nao aliwakimbilia mashabiki huku amevua jezi yake akiwa anashangilia kana kwamba amefunga bao hilo katika mechi na uwanja mzima ulikubikwa na shangwe.

Shangwe hilo halikuishia kwa mashabiki bali hata kwa viongozi waliokuwa uwanjani hapo, Barbara Gonzalez, Mohamed Nasorro, Zacharia Hans Poppe na Crescentius Magori waliinuka na kumpigia makofi.

Kama Morrison atapewa nafasi ya kucheza mechi dhidi ya Yanga itakuwa mara ya kwanza kwake tangu alipojiunga na Simba msimu huu akitokea mitaa ya Jangwani alikokuwa kipenzi.