Fei Toto, Yanga kimeeleweka

MWANASPOTI linajua kabla ya jua kuzama leo Jumatano Juni 7, Feisal Salum 'Fei Toto' atatambulishwa rasmi ndani ya Azam.

Licha ya Azam kufanya siri, lakini Mwanaspoti linajua klabu hiyo ilimalizana na Yanga jana jijini Dar es Salaam baada ya kikao kizito cha pande zote mbili.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwaomba Yanga kumaliza mgogoro na kiungo huyo Mzanzibari, ili mambo mengine yaendelea.

Fei aliingia kwenye mgogoro huo, baada ya kuvunja mkataba bila kuzingatia kanuni, hadi kesi kupelekwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) bado Yanga ikawa kwenye upande wa haki.

 Kwa habari zaidi endelea kufuatilia kwenye mitandao yetu na Gazeti la Mwanaspoti kesho Alhamisi Juni 8.