Farid amtoa Yassin kikosini

Muktasari:
- Farid ambaye nafasi yake asili ni winga ila baada ya Yanga kuwakosa mabeki wake watatu wa kushoto amekuwa akitumika katika nafasi hiyo na leo dhidi ya Kagera Sugar inakuwa ya tatu akicheza kama beki wa kushoto.
FARID Mussa amendelea kuwepo katika kikosi cha Yanga huku akitumika katika nafasi ya beki wa kushoto.
Farid ambaye nafasi yake asili ni winga ila baada ya Yanga kuwakosa mabeki wake watatu wa kushoto amekuwa akitumika katika nafasi hiyo na leo dhidi ya Kagera Sugar inakuwa ya tatu akicheza kama beki wa kushoto.
Farid alianza kucheza nafasi hiyo katika mechi ya Mbeya City iliyomalizika kwa suluhu na baada ya hapo akafuata nyingine mbili dhidi ya ikiwemo iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar.
Farid anacheza katika nafasi hiyo kutokana na kuumwa kwa Bryson Raphael, Kibwana Shomary na Yassin Mustapha ingawa yupo benchi la wachezaji wa akiba.
Yassin ameshindwa kumtoa Farid katika nafasi hiyo pengine kutokana na mambo mawili huenda akawa anawalizisha benchi la ufundi kutokana na kiwango chake au Yassin kutokuwa fiti zaidi.
Wachezaji wengine walioanza kwenye kikao cha Yanga leo, kipa Djugui Diarra, Djuma Shabani, Farid, Yanick Bangala na Bakari Mwamnyeto.
Wengine Khalid Aucho, Salum Abubakar, Denis Nkane, Dickson Ambundo, Saido Ntibazonkiza na Fiston Mayele.
Kwenye benchi la akiba wao kipa, Abuotwalibu Mshery, Paul Godfrey, Yassin, Ibrahim Bacca, Deus Kaseke, Mapinduzi Balama, Zawadi Mauya, Yusuph Athuman na Heritier Makambo.