Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fadlu anogewa Simba, atoa siri ya Ahoua

FADLU Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa takwimu, Ahoua ameshafunga mabao 15 akiwa ndiye kinara wa orodha ya wafungaji Bara, lakini akiwa na asisti saba hivyo kuhusika moja kwa moja na mabao 22, moja zaidi ya Dube ambaye ana mabao 12 na asisti tisa ikiwa na maana ya kuhusuka na mabao 21.

CHARLES Jean Ahoua, sasa ndiye mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara akimpiku mpinzani wake mkubwa kutoka Yanga, Prince Dube baada ya juzi kufunga hat-trick walipoifumua Pamba Jiji kwa mabao mabao 5-1.

Kwa mujibu wa takwimu, Ahoua ameshafunga mabao 15 akiwa ndiye kinara wa orodha ya wafungaji Bara, lakini akiwa na asisti saba hivyo kuhusika moja kwa moja na mabao 22, moja zaidi ya Dube ambaye ana mabao 12 na asisti tisa ikiwa na maana ya kuhusuka na mabao 21.

Katika mchezo uliochezwa juzi, Alhamisi kwenye Uwanja wa KMC, Ahoua alionyesha ubora mkubwa kwa kufunga mabao matatu, akiiwezesha Simba kupata ushindi mnono na kuendelea kupambana katika mbio za ubingwa dhidi ya mpinzani wake wa jadi, Yanga. Hat trick aliyofunga Ahoua inakuwa ya kwanza kwake tangu atue Msimbazi, lakini ni ya nne kwa msimu huu akitanguliwa na Dube, Stephane Aziz KI wote wa Yanga na Steven Mukwala wa Simba.

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, hakusita kumwaga sifa kwa kiungo huyo mshambuliaji, akisema kiwango chake ni cha juu kutokana na kasi aliyonayo, nguvu na maarifa ya kusoma mechi.

“Kile mnachokiona kwa Ahoua si ajali, ni matokeo ya kazi kubwa. Anafanya kazi kila siku mazoezini, anapigania nafasi yake na sasa matunda yanaonekana,”€  alisema Fadlu na kuongeza:

“Ukiangalia mabao yake, yana mchanganyiko wa uwezo binafsi yupo kwenye nafasi sahihi, anapiga ‘free kick’, penalti, pia anaona wenzake msimu mzuri kwake kwa kushirikiana na wenzake pamoja na kwamba hii ni mara yake ya kwanza kucheza ligi ya Tanzania.”€

Katika mechi 22 alizocheza, Ahoua ametumika kwa dakika 1590 akifanikiwa kuwa mchezaji bora wa mechi mara tano na kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi mara moja. Mchango wake umekuwa mhimili kwa Simba katika kipindi cha ushindani mkali wa Ligi Kuu Bara.

Kwa kulinganisha, Clement Mzize wa Yanga ana mabao 13 na asisti tatu, huku kiungo wa Azam FC, Feisal Salum akiwa na mabao manne na asisti 13, akithibitisha nafasi yake kama kiungo bora zaidi mchezeshaji kwa sasa.

Hata hivyo, Ahoua amejikita kwenye mstari wa mbele licha ya Simba kuwa na washambuliaji wa mwisho au kati kama vile Leonel Ateba mwenye mabao 12 na Steven Mukwala mwenye tisa.

Katika msimu huu, Ahoua pia ameonyesha umahiri wa kufunga mabao ya aina mbalimbali, mabao 6 kwa penalti na mabao mawili kwa ‘free kick’, jambo linalomfanya kuwa tishio pande zote za uwanja.

Kiwango cha Ahoua kimekuwa kipimo kwa washambuliaji wengine wa ligi. Ukiacha Dube, ambaye aliwahi kuongoza mbio za mfungaji bora, sasa anapata changamoto kubwa kutoka kwa Ahoua na hata Mzize, ambaye naye anaonekana kuwa na msimu mzuri.

Ahoua pia amefanikiwa kuwa sehemu muhimu ya mfumo wa mashambulizi wa Simba unaoendeshwa na viungo wengine washambuliaji kama vile Ellie Mpanzu na Kibu Denis ambao wameifanya pia timu hiyo kuwa tishio.

Kikosi cha Simba kinaonyesha kuhitaji kumaliza msimu kwa kishindo na kwa kiwango hiki cha Ahoua, matumaini ya mashabiki wa Msimbazi ni kuona kombe likirudi kwao mwishoni mwa msimu baada ya kumaliza patupu ndani ya misimu mitatu iliyopita.

Katika mahojiano na Mwanaspoti, Fadlu alisisitiza kuwa Ahoua bado hajafikia kilele cha uwezo wake: “Anaweza kufanya zaidi ya haya. Ni suala la kumsaidia aendelee kuwa na nidhamu ya kazi na kubaki na njaa ya mafanikio. Tunajivunia kuwa naye.”€Simba itashuka uwanjani kesho Jumapili kumalizia kiporo cha Ligi Kuu dhidi ya KMC kabla ya kusafiri kuifuata RS Berkane kwa pambano la kwanza la fainali ugenini litakalopigwa Morocco, Mei 17 na kurudiana Mei 25 Kwa Mkapa huku Kombe la Shirikisho Afrika likiwa uwanjani kusubiri bingwa.