Emmy Kosgei afurahia ndoa yake na budaa

MWANAMUZIKI  wa injili Emmy Kosgei kasema hajutii kuolewa na budaa ikiwa ni baada yake kusherehekea kutimiza miaka saba kwenye ndoa yake.
Kosgei alitrendi sana humu nchini 2013 alipoamua kuolewa na askofu wa Mnigeria Anselem Madubuko.
Wakati huo, Kosgei alikuwa binti wa miaka 33, huku askofu huyo akiwa ni budaa wa miaka 55. Wengi walidai kuwa Emmy aliamua kuolewa na budaa kwa sababu ya mali. Emmy alijitetea kwa kusema kuwa wanaume wachanga waliogopa kumtongoza na ni Madubuko pekee ndiye aliyepata ujasiri wa kumkatia.
Miaka saba baadaye ndoa yao ingali imesimama na Emmy anasema hajutii kuplewa na budesko huyo.
“Nikitazama miaka saba iliyopita, wala sijutii kuolewa naye. Kanitunza kama malkkia vile, kunijali na kunionyesha mapenzi ya dhabiti. Hata ikitokea miaka ikarudi nyuma bado akinijia nitamkubali” Emmy kaungama.
Kwa sasa Mandubuko ana umri wa miaka 62 huku mkewe akitimiza miaka 40. Mandubuko alimwoa Emmy baada yam ked wake wa kwanza Connie Uzoamaka kufariki dunia Julai 2018 baada ya kushikwa na mshtuko wa moyo.